November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Watanzania watakiwa kutembelea Banda WMA kupata elimu ya Mita za umeme

Na Jackline Martin, TimesMajira Online

Wakala wa vipimo wamewataka watanzania kufika katika Banda lao katika maonesho ya 48 ya biashara ya kimataifa sabasaba kupata elimu mbalimbali ikiwemo elimu ya Miata za umeme.

Wakala hao kwa sasa wanahakiki mita za umeme kuhakikisha kwamba mtumiaji wa umeme anapata UNIT sawa na matumizi yake anayotumia

Akizungumza na waandishi wa Habari Jana Jijini Dar es Salaam katika maonesho hayo, Meneja wakala wa vipimo mkoa wa Iringa, Lina msuya alisema mwananchi atajua kama Mita yake imehakikiwa na wakala wa vipimo, Mita hiyo itawekwa siri yao yenye nembo ya WMA.

“Mita tunazozihakiki ni Zile Mita mpya kabla mteja hajafungiwa na Zile ambazo zipo kwenye matumizi kwa maana ya kwamba Mita zinaponunuliwa au zinapoingia nchini kabla mteja hajafungiwa Mamlaka za maji wanazileta kwetu kwaajili ya kuhakikisha”

Aidha alisema wanapita mitaani kwa Zile Mita ambazo tayari zimefungwa kuona kwamba matumizi yake yanaendaje lengo ikiwa ni kumlinda mlaji kwa kuhakikisha mlaji analipa bili kutokana na matumizi ya maji anayotumia

Mbali na hayo Msuya alisema kupitia maonesho hayo watatoe elimu kuhusiana na kifaa hicho ambacho kinatumika kwaajili ya kuhakiki Mita hizo zilizokuwa kwenye matumizi

“Tunahakiki Mita kama zinatumika vizuri, bili anayopewa mtu kama inalingana na matumizi ya maji aliyotumia”

Pia alisema Mteja atakapopita kwenye Banda lao atapata elimu ya matumizi sahihi ya dira za maji kwani wao pia wanahakiki dira hizo.

“Ukitaka kujua kama dira hiyo imehakikiwa na wakala wa vipimo, utakuta kuna Siri ya wakala wa vipimo,”

Kadhalika katika maonesho hayo mteja atapata nafasi ya kupata elimu ya namba bora ya ufungashaji wa mazao ya shamba

“Tunaelewa kabisa sheria ya vipimo inatueleza kwamba ufungashaji wote wa mazao ya shamba lazima uzingatie sheria ambayo inasema mazao yote yafungashwe kwa uzito usiozidi kilo 100 na ukifungasha kwa uzito ulizidi kilo 100 inamaana umekiuka sheria ya vipimo”