Na Penina Malundo, Timesmajira
NAIBU Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Exaud Kigahe amewataka watanzania kuchangamkia fursa za kituo cha biashara na usafirishaji Afrika Mashariki kinachojengwa Ubungo jijini hapa kinachotarajiwa kufunguliwa Juni mwakani.
Hayo yameelezwa katika maadhimisho ya siku ya China katika maonyesho ya 47 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) ndani ya viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, amesema
kituo hicho kitakachogharimu dola za Marekani 114 milioni (zaidi ya Sh264.3 bilioni), kukamilika kwake, pamoja na shughuli nyinginezo, kitakuwa kikipokea bidhaa muhimu kutoka China zinazohitajika kwa soko la Afrika Mashariki.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho Cathy Wang amesema kufunguliwa kwa Kituo hicho kunaendana na dhamira yao ya kuwezesha Biashara za China kuingia Afrika.
“Hii inachukua nafasi kubwa katika kuimarisha mabadilishano ya kiuchumi na kibiashara, ushirikiano na kuongeza thamani kwa kuanzisha viwanda vya usindikaji vitakavyochangia ukuaji wa Tanzania ya viwanda.
Amesema kwa mujibu wa Mkakati wa uwekezaji wa China, unaosema ‘Biashara kwanza, uwekezaji ufuate’ unaweka uhakika wa kujengwa kwa viwanda vinavyozalisha bidhaa zitakazokuwa zikiingizwa nchini kupitia kituo hicho kwani tayari kutakuwa na uhakika wa soko.
Katika upande wa uchangamkiaji fursa, Naibu Waziri, Kigahe amesema ni vyema Watanzania wakatembelea banda la China ndani ya maonyesho hayo ili kujenga mtandao wa kirafiki na kampuni hizo ili waweze kufanya biashara.
“Wanaokuia kwenye maonesho haya wasiache kuingia banda la China, kujifunza teknolojia mbali mbali pia wahakikishe wanajenga mtandao mzuri wa ushirikiano, kuwashawishi kufungua makampuni yao hapa na kuzalisha bidhaa hapa nchini badala ya kufuata China,” amesema.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba