Na Mwandishi wetu, TimesMajiraUpdates
Kituo cha kudhibiti magonjwa nchini Marekani (CDC) kimewataka watanzania kutosafiri katika taifa hilo na kama kuna ulazima basi mtu awe amepata chanjo kamili dhidi ya corona.
Aidha wamesema, “hali ya sasa nchini Tanzania, hata wasafiri walio na chanjo kamili wanaweza kuwa katika hatari ya kupata na kueneza virusi vipya vya corona” CDC imesema.
Siku ya Jumapili, taarifa zilienea mitandaoni kuwa msafiri kutoka Tanzania alipimwa na kukutwa na aina mpya ya virusi vya corona- Omicron huko New Delhi, India, na kusababisha mamlaka ‘kuanza uchunguzi’.
Licha ya tahadhari za mara kwa mara kutoka kwa Wizara ya Afya ya Tanzania, uzingatiaji wa umma kwa hatua za kuzuia Covid-19 bado ukochini, Ubalozi wa Marekani umesema.
Ikumbukwe kuwa Kituo hicho cha kudhibiti magonjwa nchini Marekani (CDC) imeweka Tanzania katika orodha ya nchi hatari kusafiri.
More Stories
Ushiriki wa Rais Samia G20 wainufaisha Tanzania
Rais Samia apeleka Bil. 6 kuboresha sekta ya elimu Kaliua
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM