November 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Watanzania washauriwa kutumia usuluhishi badala ya Mahakama

Na Joyce Kasiki Timesmajira online

WANANCHI wameaswa wabadilishe mtazamo kwa kutumia usuluhishi zaidi badala ya Mahakama katika kusuluhisha migogoro ili kuokoa muda lakini kudumisha mahusiano katika jamii.

Hakimu Mkazi  pia ni Msaidizi wa Sheria wa Jaji Mahakama Kuu Kituo cha Usiluhishi Rahel Kangaga  amesema hayo wakati akizungumza kwenye maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kituo hicho na faida zake.

Amesema wananchi wanapenda kesi zao ziende kusikilizwa mahakamani mahali ambako kupoteza muda mwingi kusikiliza kesi mpaka kufikia hatua ya hukumu.

“Lakini katika kituo cha Usuhishi kwanza  kunadumisha mahusiano kwa sababu mpaka mnafikia hatua ya mwisho ya makubaliano kuna kupeana na mikono ,

“Pia inakuza uchumi, hii ni kwa sababu inatumia muda mfupi mpaka kufikia hitimisho tofauti na kesi za mahakamani ambapo husika hutumika muda mwingi kutokana na taratibu lakini kuahirishwa kwa kesi kwa mara kwa mara,

“Kwa hiyo kwa kutumia kituo hiki wahusika wanapata muda mzuri wa kufanya shughuli zao za kiuchumi.”amesisitiza Kangaga

Aidha Kangaga amesema kituo hicho kinasikiliza na kutatua migogoro yenye asili ya madai kwa kesi ambazo zinafunguliwa Mahakama Kuu au Mahakama ya Divisheni ya Ardhi.

Amesema  baada ya kesi kufikia hatua ya usuluhishi kwa amri ya Hakimu anayeisikiliza na kupeleka katika kituo hicho,wahusika ambao ni mdai na mdaiwa huitwa na kukaa kwenye meza ya mazungumzo na wanapofikia muafaka,wanasaini  makubaliano hayo ambayo kama yatakiukwa na mdaiwa  ,makubaliano hayo yatatumika kukazia hukumu.

Hakimu huyo amesema zipo kesi ambazo wanafanikiwa na kuandaa hati ya makubaliano ambayo inakuwa kama hukumu.

Amesema,kwa kipindi cha Januari -Juni kituo hicho kimetokea kesi wasanii wa 150 ambapo zilizotoka Mahakama Kuu ya Dar Es Salaam ni 66 na kutoka Divisheni ya Ardhi ni 84 ambapo kesi zilizofanikiwa ni 38 na zilizofeli ni 97.

Aidha amesema,kituo hicho kimeanzishwa 2015 ambapo imetokana na utafiti kuonesha kwamba migogoro inaweza kuisha kwa njia mbadala kabla ya kesi kufikia hatua ya kusikilizwa kimahakama.