January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Watanzania washauriwa kunywa Maziwa

Na Irene Clemence,timesmajira, Online

WATANZANIA wameshauriwa kunywa maziwa halisi ya ngombe ili waweze kuwa na afya imara.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya 46 yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Jijini Dar es Meneja Masoko wa Kampuni ya Asasi inayozalisha maziwa Jimmy Kiwelu amesema watanzania wengi awapendi kunywa maziwa kutokana na kutokujua umuhimu wake.

“Maziwa yanavirutubisho vingi katika mwili wa binadamu kwani umfanya mtu awe na afya bora na njema”amesema

Kiwale amesema miongoni mwa sababu ya watu kutokupenda kunywa maziwa ni tabia na malezi na kutokuandaliwa mapema.

Amebainisha kuwa kwa mujibu wa Shirika la WHO limeeleza kuwa kitaalamu binadamu anapaswa kunywa maziwa lita 50 .

“Bado tunayokazi kubwa ya kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kunywa maziwa yanavirutubisho vingi ndani ya mwili wa binadamu”amesema

Kiwale amesema katika kutambua umuhimu wa maziwa kwa binadamu Kampuni hiyo imekuwa ikisindika katika ujazo mbalimbali ili kila mtanzania aweze kumudu gharama.

Amendelea kueleza kuwa Kampuni hiyo ambayo makao makuu yake Iringa inazaidi ya wafugaji 6000 ambao wako katika nyanda ya juu kusini.

Kiwale amesema maziwa ambayo yamekuwa yakizalishwa ni halisi na ya ngo’mbe na yamekuwa yakisindikwa na kuwekwa katika ujazo mbalimbali.

Aidha amewakaribisha Wananchi kutembelea katika banda lao ili waweze kijifunza na kuona Mambo mbalimbali ambayo yamekuwa yakizalishwa na kampuni hiyo.