November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Watalamu wa afya watakiwa kusimamia maadili

Na Queen Lema, TimesMajira Online, Arusha

Watalamu wa sekta ya afya hususani wauguzi hapa nchini wameaswa kuhakikisha kuwa wanatumia vema taaluma yao ikiwa ni pamoja na kuwa na lugha nzuri Kwa wagonjwa na kuepukana na tabia ya kuwa na maadili mabaya.

Hayo yameelezwa na mchungaji Godson Abeli ambaye ni msaidizi wa Askofu wa kanisa la Kkkt dayosisi ya kaskazini Kati wakati akiongea kwenye maafali ya 8 cha Chuo cha uuguzi na sayansi ambacho kipo chini ya kanisa la Kkkt dayosisi ya kaskazini kati.

Mchungaji Godson alisema kuwa Kwa sasa kuna baadhi ya wauguzi ambao wanalalamikiwa vyema na wanaacha kufuata taaluma Ambayo wameipata kutoka kwenye vyuo.

Alisema kuwa wauguzi hao wanashusha thamani ya taaluma hiyo Ambayo ni muhimu Sana kwenye jamii kwa kuwa wanaokoa maisha ya watu wengi.

“Nawasihi Sana hawa wauguzi ambao Leo ni waitimu wahakikishe kuwa wanakuwa sehemu ya uzalendo wa Taifa kwa kufuata maadili lakini pia kuwa na roho ya kizalendo na kuachaana na tabia ya kutoa lugha chafu Kwa wagonjwa”alisema

Awali kaimu mkurugenzi wa Arusha Lutheran Medical center Dkt Goodwill Kivuyo alisema kuwa chuo hicho cha sayansi kina mikakati mbalimbali ambayo itaweza kuwasaidia wanafunzi ambao wanatamani kusoma elimu hiyo ya uuguzi.

Dkt Kivuyo alisema pamoja na mikakati walionayo lakini bado wanaitaji wahisani ambao wataweza kuwashika mikono kwa kuwa chuo hicho kina tumia mbinu mbalimbali katika kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata utofauti na vyuo vingine.

Awali Mkuu wa chuo hicho cha afya na sayansi shirikishi Lilian Shuma alisema kuwa wameweza kutoa wanafunzi 35 ambao sasa watakuwa ni wauguzi makini sana na wataweza kusimamia ipasavyo maadili katika sekta ya afya.

Shuma alisema kuwa wataendelea kufanya mikakati ya kusisitiza umuhimu wa wauguzi kufanya Kazi kwa weledi ili kuifanya sekta ya afya iweze kuwa Bora zaidi