Na Queen Lema, TimesMajira Online, Arusha
Wito umetolewa kwa watanzania pamoja na jamii kuhakikisha kuwa kamwe hawaingilii hifadhi za barabara ambazo zimetengwa kwani kwa kufanya hivyo wanavunja na kuharibu sheria za barabara.
Hayo yameelezwa jana na Aisha Malima ambaye ni Kaimu Afisa habari kutoka wakala wa barabara nchini (TANROAD) kwenye mkutano wa wadau wa usafirishaji unaoendelea Arusha
Malima alisema kuwa wapo baadhi ya wananchi ambao wanafuata na kujenga ndani ya hifadhi ya barabara kabisa hali ambayo wakat mwingine inasababisha madhara makubwa sana.
Alifafanua kuwa hifadhi za barabara zinapofuatwa na kuharibiwa au kujengwa inaweza kuwa na madhara makubwa kwa jamii yote ambapo hata majanga yanapotokea yanaweza kuleta madhara makubwa sana.
Aliongeza kuwa hifadhi za barabara zipo kwa ajili ya upanuzi na matumizi mengine na ndio maana zikaachwa na kwa mujibu wa sheria hazitakiwi kuharibiwa au kufanyiwa matumizi mengine.
Katika hatua nyingine alimshukuru Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samiah Suluhu Hasani kwa kuweza kuwapa bajeti ya matengenezo ya dharura ambayo imeweza kuwa msaada mkubwa sana.
“ukiangalia hata katika majanga ambayo yametokea huko Hanang Manyara unaweza kuona kuwa tulipopata taarifa tuliweza kuanza safari papo kwa hapo na tulifika na tukaanza kazi mara moja ili kuweza kuruhusu shuguli nyingine ziweze kufanyika kwa haraka”aliongeza
Alihitimisha kwa kuwataka wananchi kuhakikisha kuwa wanapoitaji msaada wowote ule kamwe wasisite kuuliza ili waweze kuwa sawa kwa mujibu wa sheria kanuni na taratibu za nchi.
More Stories
Ushiriki wa Rais Samia G20 wainufaisha Tanzania
Rais Samia apeleka Bil. 6 kuboresha sekta ya elimu Kaliua
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM