December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Watakiwa kutoa huduma kwa kuzingatia utu

Na Esther Macha, TimesmajiraOnline,Mbeya

WATAALAMU wa afya katika hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya wametakiwa kutoa huduma za afya kwa kuzingatia utu pindi wanapotoa matibabu kwa wagonjwa pamoja na kuonyesha upendo na kuwa  upendo una nguvu kuliko hata dawa wanazotumia.

Kauli hiyo imetolewa leo,Februari 21,2024 na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya Dkt.Godlove Mbwanji  wakati akifungua mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uwezo zaidi wahudumu wa afya watarajali katika eneo la utaoji wa huduma za matibabu kwa wagonjwa wanaoishi na virusi  ya  ukimwi.

Michael Mwagala ambaye ni maratibu wa mafunzo hayo amesema mafunzo hayo ya siku tatu yamehusisha watoa huduma za afya watarajali wakiwemo, Madaktari, Wauguzi pamoja na watalaamu wa maabara na kuendeshwa na wakufunzi kutoka Idara mbalimbali hospitalini hapo.

“Mafunzo haya yanahusisha wawezeshaji kutoka idara mbalimbali hospitalini hapa kwaajili ya kuwajengea watarajali hawa uwezo zaidi wa kuwahudumia wagonjwa wanaoishi na virusi vya ukimwi ” amesema  Mwagala

George Andrew ambaye ni kiongozi wa watoa huduma za afya watarajali hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya ameushukuru Uongozi wa hospitali na kusema mafunzo hayo yatakayofanyika kwa muda wa siku tatu yatakuwa msaada katika utendaji wao utoaji huduma za matibabu kwa wagonjwa hao wanaoishi na virusi vya ukimwi.

“Naami tumepokea mengi ambayo yamezungumzwa na yatatusaidi katika utendaji wetu hivyo tutafanya kazi kwa bidii na kwa uaminifu kwa kuyazingatia yale tuliyoambiwa”amesema Andrew.