Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), Mhe. Augustine Vuma ametoa Rai kwa watanzania kuwa wajiandae kuanza kutumia miundombinu ya Treni ya Kisasa kuanzia mapema 2024.
Vuma ametoa rai hiyo wakati wa ziara ya wajumbe wa Kamati hiyo ya kukagua miundombinu ya njia ya kusafirisha umeme katika Reli ya Kisasa(SGR), tarehe 18 Desemba, 2023 mkoani Morogoro.
Vuma amesema Watanzania wanatakiwa kuanza kujiandaa kutumia fursa za kiuchumi ikiwemo kusafirisha bidhaa mbalimbali ikiwemo mazao pia wao wenyewe kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa kuwa Serikali imetumia Mabilioni ya fedha kuhakikisha mradi huo unatekelezeka na kukamilika kwa wakati.
“Kuna kaulli inasema hakuna kilichosimama, pia kuona ni kuamini! kweli tumekuja kuangalia na tumeona hakuna kilichosimama, Ujenzi wa Miundombinu ya umeme katika Reli hii umeenda kwa kasi sana, tunaimani kwamba Watanzania watanza kutumia Reli hiii ya Kisasa mapema mwakani kama ilivyopangwa, tunaipongeza Serikali inayoongozwa na Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za kutekeleza Mradi huu”, alisema Mhe. Vuma.
Amesema Kamati hiyo imeona utekelezaji wa miundombinu hiyo na uwekezaji Mkubwa uliofanyika hivyo imejihakakikishia na kuthibitisha kuwa kuanzia mwakani Watanzania wataanza kutumia treni hiyo, kutokana na kazi kubwa iliyofanyika na kukamilika.
Vilevile Wizara ya Nishati kwa kushirikiana na Wizara ya Uchukuzi kupitia taasisi husika zitafanya kazi kwa bidii na kusimamia fedha za Serikali kuhakikisha zinatumika vizuri katika miradi.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga, amesema ziara hiyo ni maelekezo ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko ya kutaka waheshimiwa wabunge watembelee miradi hiyo kwa lengo la kuona, kukagua na kutoa ushauri kwa Wizara husika juu ya utekelezaji wa miradi hiyo kwa kuwa imamaslahi makubwa kwaTaifa.
Mhe. Kapinga amesema dhamana waliyopewa ni kusimamia mradi huo kwa kushirikiana na Shirika la Reli nchini (TRC), hivyo wanafanya kazi hiyo kwa weledi mkubwa, kuhakikisha fedha zinatolewa na Serikali zinatekeleza miradi hiyo kwa wakati ili kufanikisha kuanza kutumika kwa treni hiyo ya kisasa ambayo ni moja ya maeneo yatakayoleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi kwa Taifa.
Amesema tayari mradi huo umetembelea na kamati mbalimbali ikiwemo Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma.
Mradi huo kutoka Dar es salaam hadi Morogro umekamilika kwa asilimia 100, na Morogoro hadi Dodoma asilimia 99, mradi umebakiza asilimia moja ili kukamilika kutoka Dar es salaam hadi Dodoma.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi