Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Watafiti wa vyuo vikuu hapa nchini wameaswa kuendelea kufanya utafiti kwenye michoro ya miambani ya kolo kondoa ili kuwezesha upatikanaji na ufumbuzi wa mambo mbalimbali ambayo yalichorwa Kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kizazi kijacho.
Aidha mpaka sasa kuna mawe 1000 ambayo bado yanatakiwa kufanyiwa utafiti wa kwenye michoro ya miambani Kolo Kondoa Dodoma huku yaliyofanyiwa utafiti pekee ni 480
Hayo yameelezwa na Amoni Mgimba ambaye ni mhifadhi daraja la kwanza,kutoka katika kituo cha michoro ya miambani Kolo Kondoa wakati akizungumza na waandishi wa habari ambao walitembelea vivutio mbalimbali wiki iliyopita
Mgimwa alisema kuwa vivutio vya michoro ya miambani ni moja ya vivutio ambavyo vimekuwa vikionesha mambo mbalimbali hasa ya kizazi cha kale
Alisema kuwa kupitia michoro hiyo ya mapangoni fursa nyingi sana zimeweza kuibuliwa huku Jamii pamoja na taifa ikipata faida
“Tunaweza kuona faida ambayo vivuo hivo vimepata moja ni kutangaza Tanzania Duniani sasa utafiti ukiwa umekamilika Kwa mawe hayo 1000 tutafika mbali sana “aliongeza
Mhifadhi huyo alisema kuwa mpaka sasa mawe ambayo yamechorwa yapo Zaidi ya 480 natayari imefanyiwa tathimini na watafiti toka ndani na nje ya nchi huku miamba mingine 1000 ikiwa bado inaitaji utafiti
Katika hatua nyingine alisema kuwa michoro hiyo ya miambani inawakilisha urithi unaoishi(the Living Heritage)hivyo hata watanzania nao wanatakiwa kutembelea vivutio hivyo
“Sisi tunaweza kusema kuwa hapa tuna Utalii kama Utalii lakini pia Utalii huu imebeba maana halisi ya utamadani hasa wa watanzania na ndio maana waliochora waliochora ili kuifadhi Mila na desturi”aliongeza
Aliwataka hata watanzania kuhakikisha kuwa wanatembelea na kutangaza vivutio na kuwa sehemu ya Utalii na kuachana na tabia ya kuona wanaostaili Utalii ni watu wa nje ya nchi pekee.
More Stories
Wananchi Babati wamshukuru Rais Samia kwa kuwafungulia barabara
Rais Samia aungwe mkono ajenda ya nishati safi ya kupikia
Ushiriki wa Samia G20 wainufaisha Tanzania