November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wataalamu waaswa kupeleka Teknolojia ya Mifugo na Uvuvi Vijijini

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule amewahasa wataalamu wa mifugo na uvuvi kupelekea na kufundisha teknolojia ya mifugo vijijini ili kuwapa wafugaji elimu ya kutosha kuhusu ufugaji wa kisasa kwa lengo la kuleta tija katika sekta hiyo.

Akizungumza, Agosti 4, 2024 mkoani Dodoma alipotembelea kwenye Maonesho ya Nanenane ya Kimataifa yanayofanyika Kitaifa mkoani Dodoma katika mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Senyamule amesema wataalamu wahakikishe teknolojia hii inawafikia wadau wote wa mifugo na uvuvi, ususani maeneo ya vijijini.

“wataalamu wachukue hatua ya kwenda kwenye makundi ya wafugaji ili kwenda kuwaelimisha kuhusu teknolojia mpya ya ufugaji na kuhakikisha inawafikia” amesema Mhe. Senyamule

Aidha, Mhe. Senyamule alisema serikali ya awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, imefanya mapinduzi makubwa sana katika sekta ya Mifugo na Uvuvi kwani ameshuhudia teknolojia mbalimbali na nzuri katika mabanda ya Mifugo na Uvuvi.

Mhe. Senyamule alisema ata sekta binafsi pia wamepokea mabadiriko hayo ya kiteknolojia, ususani upande wa vijana wa Jenga Kesho iliyo Bora (BBT) ambao wanatumia teknolojia hizi kama ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba.

Vilevile Mhe. Senyamule ametoa wito kwa wadau wote wa Mifugo na Uvuvi kutumia fursa hii ya maonesho haya ya nanenane ili kuweza kujifunza na kupata ufahamua juu ya teknolojia hii ya mifugo na uvuvi.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, (wa kwanza kulia), akielezewa na Afisa maendeleo ya jamii wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Beatrice Mwijage (wa kwanza kushoto), juu ya Mpango wa unywaji Maziwa Shuleni, mara baada ya kutembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ni katika Maonesho ya Nanenane ya Kimataifa yanayofanyika Kitaifa Mkoani Dodoma, Agosti 4, 2024, Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule (kushoto), akielezewa na Mnufaika wa vizimba vya kufugia Samaki, Bw. Omary Mangu (wa kwanza kulia), juu ya Programu ya Ufugaji samaki kwa njia ya vizimba, ni katika Maonesho ya Nanenane ya Kimataifa yanayofanyika Kitaifa Mkoani Dodoma, Agosti 4, 2024, Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule (wa tatu kulia), akizungumza na watendaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kutoka Idara ya Nyanda za Malisho (DGLF), ni katika Maonesho ya Nanenane ya Kimataifa yanayofanyika Kitaifa Mkoani Dodoma, Agosti 4, 2024, Dodoma.