January 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wataalam wa Maendeleo ya Jamii watakiwa kuifanya taaluma hiyo kuwa kamili inayotambulika kisheria

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Wataalam wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum, wametakiwa kuifanya taaluma hiyo kuwa taaluma kamili inayotambulika kisheria.

Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum Dkt Dorothy Gwajima wakati akizungumza na baadhi ya Wajumbe wa Chama cha Wataalam wa Maendeleo ya Jamii (CODEPATA) ya Jamii Gwajima Mei 06, 2022 jijini Dodoma .

Dkt. Gwajima alisema uwepo wa Sheria ya kuundwa kwa Taaluma ya Maendeleo ya Jamii itasaidia Taaluma ya Maendeleo ya Jamii kuwa na nguvu kwenye utekelezaji wa majukumu yao katika Mikoa Halmashauri.

Ameongeza kuwa changamoto wanazopitia Watalaam wa Maendeleo ya Jamii ikiwepo watu wasio wanataaluma kupangiwa majukumu ya Maendeleo ya Jamii hivyo uwepo wa Sheria itasaidia kutatua changamoto hizo zilizopo.

“Taaluma ya Maendeleo ya Jamii lazima uwe kwamujinj Sheria ikawa na Bodi na Mamalka yake itasaidia kutatua changamoto nyingi zianawakabiki wataalam hawa na jamii yetu pia ” alisema Dkt Gwajima

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt Zainab Chaula alisema Wataalam wa Maendeleo ya Jamii wanapaswa kuwa chachu ya maendeleo na mabadiliko ya fikrsa na kusaidia Jamii kutatua changamoto zinazowakabili kwa kuwapa ufumbuzi na namna ya kukabiliana nazo.

“Ukipita katika mitaa huko tunaona watu wengi wanapambana maisha hasa Wanawake hao ndio wetu tuwasaidie kutatua changamoto zao ili wajikwamie kiuchumi” alisema Dkt Chaula

Naye rais wa Chama cha Wataalam wa Maendeleo ya Jamii (CODEPATA) Angela Mvaa ameshukuru Waziri Dkt. Gwajima kwa nasaha na maelekezo yake na Chama hicho kitahakikisha kianweka nguvu ya kuwa na sheria ambayo itabadilisha kabisa mtazamo na uelekea wa Taaluma ya Maendeleo ya Jamii nchini.

Wakati huo huo Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum Dkt. Dorothy Gwajima amekutana na kuzungumza na Chama cha Wataalam wa Ustawi wa Jamii nchini waliofika ofisini kwake kujadiliana namna ya kuboresha kada hiyo katika kuisadia jamii kupambana na changamoto mbalimbali.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na baadhi ya Wajumbe wa Chama cha Wataalam wa Maendeleo ya Jamii (CODEPATA) katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt Zainab Chaula akizungumza katika kikao cha Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum Dkt. Dorothy Gwajima na baadhi ya Wajumbe wa Chama cha Wataalam wa Maendeleo ya Jamii (CODEPATA) katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Patrick Golwike akifafanua jambo katika kikao cha Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum Dkt. Dorothy Gwajima na baadhi ya Wajumbe wa Chama cha Wataalam wa Maendeleo ya Jamii (CODEPATA) katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma.
rais wa Chama cha Wataalam wa Maendeleo ya Jamii (CODEPATA) Angela Mvaa akielezea vipaumbele vya Chama hicho katika kikao cha Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum Dkt. Dorothy Gwajima na baadhi ya Wajumbe wa Chama cha Wataalam wa Maendeleo ya Jamii (CODEPATA) katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma.
Baadhi ya Wajumbe wa Chama cha Wataalam wa Maendeleo ya Jamii (CODEPATA) wakimsikiliza Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum Dkt. Dorothy Gwajima katika kikao na Wajumbe wa hao katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma.