Na Mwandishi wetu,Timesmajira
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amesema ni marufuku kwa vyama upinzani kuwatumia vijana kutoka mkoani Mara kama nguvu kazi ya kufanya vurugu katika maeneo mbalimbali.
Amesema CCM inamipango mizuri kuhakikisha vijana hao wanatumia nguvu zao kujiletea maendeleo ya kiuchumi na kujikwamua dhidi ya umasikini.
Wasira ameyasema hayo leo, alipokuwa akizindua ofisi ya CCM Kata ya Nyakonga wilayani Tarime, Mkoa wa Mara.
‘Nataka niwaambie wananchi wa Tarime CHADEMA wakitaka kufanya fujo mahali popote wanakuja kuchukua vijana Tarime…wanapelekwa kufanya fujo kama majeshi ya kukodi, wakitaka kufanya fujo Mbeya wanakuja, Tarima, wakitaka kufanya fujo sehemu Tarime.
![](https://timesmajira.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/2-5-1024x683.jpg)
“Tunawaambia vijana wa Tarime wana mvua wana jua na Tarima panalimika, kila kitu kinaota tuwasaidie vijana wa Tarime watumie fursa zilizopo…tunawaambia CHADEMA muache kuja kuchukua vijana Tarime, sisi sio eneo la mapambano, vijana wetu sio wa kukodisha kwenda katika mapambano, nasema kama mzee wa Tarime waache kuja kuchukua vijana wa Tarime.
![](https://timesmajira.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/1-3-1024x683.jpg)
Wasira aliwataka vijana wasikubali kuchukuliwa na kutumika katika vurugu kwa kuwa wakienda huko hupigwa, kuumizwa na hata kupata ulemavu kisha kurudishwa Tarime wakiwa na hali mbaya.
“Nasema kama mzee wa Tarime, Mzee wa kimila, muache mambo haya mimi najua yanafanyika siku nyingi,” amesema.
More Stories
Rais Samia amlilia Dkt. Sam Nujoma
Samia ashusha neema ya kilimo cha umwagiliaji
Kasulu FC mabingwa mashindano Khimji 2025