February 12, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wasira:Uchaguzi Mkuu utafanyika wanaCCM,Wananchi jiandaeni

Na Mwandishi Wetu,Timesmajira, Mwanza

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema uchaguzi nkuu wa mwaka huu utafanyika kama ulivyopangwa na kwamba hakuna chombo cha serikali wala chama cha siasa chenye mamlaka ya kuuahirisha.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Stephen Wasira, ameyasema hayo leo Februari 11, 2025 alipohutubia mkutano mkutano wa Chama katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Wasira amesema watu wanaotoa hoja kwamba uchaguzi mkuu hautafanyika hadi yafanyike mabadiliko ya Katiba wanajisumbua kwa kuwa makubaliano yalishafanyika madiliko ya Katiba yatafanyika baada ya uchaguzi, hivyo hakuna anayeweza kuahisha kufanyika kwa uchaguzi mkuu kwa namna yoyote.

“Tumekubaliana tumalize uchaguzi, zile sheria za uchaguzi zifanyiwe marekebisho, wabunge wanajua sheria ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani imepitishwa na Bunge, sheria ya vyama vya siasa imefanyiwa marekebisho na imepitishwa na Bunge.

“Chadema wamekuwa na msemo wao maarufu ‘no reform no election’ (kama hakuna mabadiliko hakuna uchaguzi), sasa mimi hapa nasema leo uchaguzi mkuu lazima utafanyika. Wanaosema uchaguzi hautafanyika mpaka mabadiliko yafanyike wanajisumbua, uchaguzi utafanya na Watanzania wajiandae.
“Sisi ni Chama cha siasa lazima tufanye uchaguzi ili tuendelee kuleta maendeleo ya Watanzania. Halafu wamekuwa wakisingizia CCM tunaiba kura wakati hata katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2024 wameshindwa kuweka wagombea. Tunawaambia hatuna tunachoogopa,” amsema.

Amesisitiza kuwa sio chombo cha serikali wala chama cha siasa ambacho kina uwezo wa kuhairisha uchaguzi na kufafanua kuwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kisheria inalo jukumu la kutangaza tarehe ya uchaguzi, lakini haina uwezo wa kuhairisha.

“Na kama kutakuwa sababu ya uchaguzi mkuu kusogezwa mbele au kuahirishwa basi ni kwa sababu ya uwepo wa vita lakini kwa bahati nzuri nchi yetu haina vita, iko salama na kazi ya kuleta maendeleo inaendelea. Hivyo hakuna chama cha siasa kinaweza kuahirisha uchaguzi na kuhusu suala la mabadiliko ni la kisheria