December 29, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Washindi kampeni ya ‘Chawote’ kujikwamua kiuchumi

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Washindi wa zawadi ya shilingi milioni moja katika kampeni ya Chawote kutoka mtandao wa Tigo wamesema zawadi walizozipata zitawasaidia kujikwamua kiuchumi.

Wakizungumza wakati wa kukabidhiwa zawadi zao leo Julai 14 jijini Dar es Salaam ,Mshindi Kurwa abdllah ambaye ni mama lishe kutoka kigamboni Dsm amesema fedha hizo zitaongeza thamani kwenye biashara yake huku Retuta Matei anayefanya biashara ya kuuza mkaa Mabibo Dar es Salaam akisema fedha hizo zimemfika wakati muafaka.

Kwa upande wao washindi wengine fatuma Khatibu mkazi wa buza anaefanya biashara ya Saluni amesema fedha hizo zitamsaidia pakubwa kutanua wigo wa biashara yake kauli iliyoungwa mkono na mshindi mwingine Peter okoka mwasandube kutoka kurasini Dar es Salaam.

Kampuni ya Tigo imekuwa ikitoa zawadi mbalimbali kwa watumiaji wa huduma mbalimbali za mtandao huo katika kampeni maalumu ya Chawote inayotarajiwa kudumu kwa siku 90.