January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waombwa kuchangia watoto wenye ulemavu wa miguu kifundo

Na Esther Macha,Timesmajira,Online, Mbeya

MKURUGENZI wa hospitali ya Rufaa kanda ya Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji amesema kuwa ili huduma ya matibabu kwa watoto wenye ulemavu wa miguu kifundo uweze kuwa endelevu na wa kudumu ni lazima watanzania ,wafanyabiashara ,taasisi zisizokuwa za kiserikali kuchangia matibabu hayo katika sehemu yao ya huduma za kijamii katika kusaidia watoto wenye ulemavu .

Mkurugenzi wa hospitali ya rufaa kanda ya Mbeya Dkt.Godlove Mbwanji akizungumza wakati wa maadhimisho hayo

Amesema wadau ambao wamekuwa wakijitoa kulipia huduma hiyo ili kufanikisha matibabu hayo kwa watoto wenye ulemavu wa miguu kifundo hivyo tuwaombe makampuni na viwanda katika ile sehemu ya huduma kwa jamii waone namna ya kushirikiana na hospitali mbali mbali ili kuweza kutoa michango yao na fedha hizo zitolewe kwa uwazi na uadilifu ili waweze kuwahuduma wale ambao ni Taifa la kesho.

Dkt.Mbwanji amesema hayo jana wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Miguu Kifundo Duniani ambapo maadhimisho hayo yamewashirikisha wazazi pamoja na watoto wenye ulemavu wa miguu kifundo ambayo yamefanyika katika hospitali ya rufaa ya kanda ya Mbeya .

Akizungumzia kuhusu wazazi wanaoficha watoto wenye ulemavu wa miguu kifundo alisema kuwa kuna watoto wengi wanazaliwa kwenye jamii lakini wanafichwa wakati wengine unakuta wazazi hawaelewi nhivyo kuamua kuficha.

Mratibu wa miguu Kifundo Nyanda za jJu Kusini ,Veronica Marishay

“Ndugu zangu waandishi wa habari muendelee kutusaidia kutoa elimu kwa jamii ,viongozi wa dini wanakutana na watu mbali mbali kwenye nyumba za ibada ,lakini tuna viongozi wetu wa kisiasa na kijamii wote tushikishirikiane kuhakikisha kuwa wale watoto wanaozaliwa wakiwa na ulemavu wa miguu kifundo mara wanapozaliwa waelekezwe hospitali ya rufaa ya kanda mbeya ,tuwatake wananchi wasiwafiche hawa watoto huduma zipo hospitali hapa “amesema Mkurugenzi huyo.

Kwa upande wake Mratibu wa Miguu ,Kifundo Nyanda za Juu Kusini ,Veronica Marishay amesema kuwa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya imeweza kuhudumia watoto wenye ulemavu wa miguu kifundo 463 toka kuanzishwa kwake kwa ushirikiano na TCCO tangu mwaka 2015.

Aidha mratibu uyo amesema kuwa pia hospitali ya rufaa imeweza kushirikiana na hospitali zikiwemo hospitali za umma na binafsi na kuweza kuwahudumia watoto wapatao 1,450 mpaka sasa.

Hata hivyo Marishay amesema kuwa kumekuwa na changamoto za kuwepo9 kwa uelewa mdogo wa wazazi wa utambuzi wa mtoto anaezaliwa na miguu kifundo hivyo kuchangia kusababisha watoto kuchelewa kupatiwa matibabu.

Alisema suala linguine ni uwepo wa imani potofu kwa jamii kuhusiana na watoto wanaozaliwa na miguu kifundo hivyo kuchangia kujiingizaa kwqenye mambo ya ushirikina na kucheleweshewa matibabu ,pia kukosekana kwa huduma ya upasuaji kwa watoto wanaofika hospitali wakiwa wakubwa hivyo kufanya wabakie na tatizo la ulemavu wenye uwezo wa kifeda husafiri jkwenda Jijini Far es Salaam kwa ajili ya upasuaji .

Akitoa ushuhuda wa mtoto wake ambaye alizaliwa na ulemavu wa miguu kifundo ,Stephano Simfukwe amesema kuwa alianza matibabu mfufulizo kwa kipindi cha miaka mitano mpaka sasa mtoto huyo amepona na miguu imenyooka vizuri na anavaa viatu vizuri.

“Napenda kuwashauri wazazi ukiona mtoto amezaliwa akiwa na ulemavu mshauri aje hospitali ya rufaa kutibiwa matibabu ni bure ndugu zangu tusifiche watoto wenye ulemavu wa miguu kifundo”amesema mzazi huyo.

Mwisho.