December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wanu:Wazazi na walezi mnawajibu kuhimiza watoto wakike kusoma masomo ya sayansi

Na Penina Malundo,timesmajira, Online

MBUNGE  wa Viti Maalum kutoka Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti na Mwanzilishi wa Taasisi ya Mwanamke initiative,Wanu Hafidh Ameir amesema sayansi inaumuhimu kwa mtoto wa kike hivyo wazazi na walezi wanawajibu wa kuwahimiza watoto wao hao kuhakikisha wanasoma masomo hayo.

 Pia amesema ni vefma Wizara ya Elimu ikawapa kipaumbele watoto wakike wanachukua masomo na wale wanaofanya vizuri katika masomo hayo  kuwawezesha kutimiza ndoto zao.

Kauli hiyo aliitoa juzi jijini Dar es Salaam,wakati akiongea na wandishi wa habari katika maadhimisho ya siku ya Mwanamke Afrika (Pan  African Women’s day)yaliyoandaliwa na Taasisi mbalimbali ikiwemo Hudefo na Women Level  kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu,Sayansi na Utamaduni (UNESCO).

Amesema watoto hao wa kike wakisaidiwa kusimamiwa ipasavyo wanauwezo wa kufika juu na kutimiza ndoto zao ambazo wanazotamani kufikia.

“Sayansi inaumuhimu sana kwa mtoto wa kike na kuna umuhimu mkubwa sana wa kuhimiza watoto wa kike kusoma sayansi,Nashukuru wenzetu wameanza kuonyesha nguvu ya kufanya sayansi ni kitu cha kawaida kwa wasichana kusoma na sisi tutahimiza kuendelezwa kwa watoto hao hususani huko juu,”amesema Wanu

Baadhi ya viongozi wakifatilia mazungumzo mbalimbali namna ya kumuwezesha mtoto wakike katika masomo ya sayansi.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Asasi isiyoya kiserikali ya  Human Indignity Environmental Foundation (HUDEFO),Sara Pima amesema wamewakutanisha wanawale  kutoka tasnia mbalimbali ambazo ni za kisayansi na kijamii kwa lengo la kuonesha umuhimu wa sayansi kwa mtoto wa kike.
Amesema kila mtu anaweza kuwa mwanasayansi ikiwemo ile ya kuelimisha jamii na kutatua changamoto katika jamii zinazojitokeza hivyo ni vema kuwalea watoto katika misingi ya kupenda sayansi.

”Tunaunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan tunaona namna Rais Samia  anavyosisitiza, Mwanamke kujiendeleza katika masomo ya sayansi hadi kupelekea  kujenga shule katika kila halmashauri kwa lengo la kuonyesha wanawake wanaosoma sayansi wakimaliza Shule wanaweza wakaendelea katika shule hizo zilizojengwa,”anesema na kuongeza.

”Kwa sasa dunia inapokwenda  ni ya kisayansi hivyo  tukipata wataalamu mbalimbali wa sayansi wanaweza kutatua matatizo yaliyopo katika jamii yetu, na miongoni mwa fursa iliyojitokeza ni kuingiza sayansi katika malezi,”amesema.

Aidha Pima amesema wanawake wengi au vijana wameishia ndoto zao njiani  kutokana na malezi ,mifumo na mila mbalimbali walizokumbana nazo ambapo zimekuwa kikwazo cha kusababisha wanawake wengi wasifikie ndoto zao za kuwa wanasayansi.

“Kwa kuanza tunatarajia kuwa na  vipindi vya kuwalea wanasayansi kuanzia nyumbani kama UNESCO ilivyotuhaidi na  hii ni fursa nzuri kwa kuanza nayo kuhakikisha sayansi inaanzia chini,”amesema.

Naye Ofisa Programu ya Sayansi Asilia kutoka UNESCO,Keven Robert amesema, siku ya mwanamke Afrika inalenga kukumbuka na kutambua ushiriki wa wanawake katika ukombozi wa bara la Afrika kwa kipindi hicho.
 
Amesema wanafanya  maadhimisho haya kwa lengo la  kutambua na kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika masuala  mbalimbali ya kiuchumi.

“UNESCO inashiriki  shughuli hizi kwa sababu tuna agenda ya kuhamasisha ushiriki wa mwanamke, watoto wa kike pamoja na vijana katika masuala ya sayansi,teknolojia na ubunifu hivyo  tumeshirikiana  na taasisi zingine katika maadhimisho haya ili kuadhimisha siku hii kwa pamoja,”amesema na kuongeza.

”Tunamradi unaosimamia mambo kumi ikiwemo suala la tafiti ya sayansi ambayo ikifanyika inaleta  matokeo yenye  faida kwa nchi,ambayo yanasaidia kuja na mbinu mpya au zao jipya,”amesema.
Â