December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wanunuzi Morocco Square wakabidhiwa nyumba

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula, wakati wa kukabidhi mfano wa ufunguo wa nyumba alizowakabidhi wanunuzi wa Nyumba katika mradi wa Morocco Square leo Julai 01, 2023 jijini Dar es Salaam.

Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online DSM

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula amewakabidhi wanunuzi wa nyumba kwenye mradi wa Morocco Square ambao utaenda kuwa chachu ya maendeleo nchini kwa kutoa fursa mbalimbali kwa Watanzania katika kuinua uchumi na kuchangia pato la Taifa.

Katika kuunga mkono Juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan mradi huo wa Morocco Square nyumba 43 kati ya 100 zimepata wanunuzi na wamekabidhiwa nyumba zao tayari kuendelea na shughuli kwenye mradi huu mkubwa na wa mfano kwa Tanzania na Afrika mashariki.

Akizungumza wakati wa kukabidhi nyumba hizo kwa wanunuzi leo Julai 01, 2023 jijini Dar es Salaam Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula ameyataka mataasisi mbalimbali kuungana na shirika la nyumba la Taifa (NHC) katika kuhakikisha wanabadiliaha mandhari ya miji ya nchi yetu.

Aidha, niwapongeze watu wa kariakoo ambao walipata taharuki kusikia kuwa kuna wawekezaji wanaoingia ubia na shirika la nyumba la Taifa (NHC) lakini baada ya kulielewa somo wao pia Sasa wamekuwa mabalozi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa ( NHC) Hamad Abdallah, amesema kuwa mradi huo unasehemu mbalimbali ikiwemo hoteli na vingine vingi ambavyo vinaendana na sehemu za nchi nyingine duniani ambazo tayari zimeshaendelea ikiwemo Marekani.