Na Mwandishi Wetu,TimesMajira Online
WANAWAKE nchini wameaswa kuwekeza zaidi katika kilimo cha kisasa ili waweze kunufaika kiuchumi kupitia shughuli hizo.
Akizungumza katika maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF) maarufu Sabasaba yenye kauli mbiu ‘ Uchumi kwa Ajira na Biashara Endelevu’ Meneja wa Kampuni ya Umma inayojiusisha na Wakulima kufanya Kilimo Biashara, JATU Plc Mohammed Simbano amesema wanawake wanatakiwa kuwekeza zaidi katika kilimo kwa ajili ya manufaa ya na Taifa kwa ujumla.
Amesema kampuni ya JATU Plc imefanikiwa kuwekeza zaidi katika baadhi ya Mikoa na Wilaya na kufungua viwanda ambavyo vinapokea mazao hayo ya mikakati.
Simbano amesema lengo la JATU PLc ni kuwainua wanawake na wananchi waliowekeza katika kilimo ili wanapovuna mazao yao wayapeleka katika viwanda vilivyopo karibu nao.
“Lengo letu ni kuwainua wanawake na wananchi kwa ujumla wanapovuna mazao wanajua wanayapeleka wapi kwa ajili ya kupatiwa masoko”,amesema Simbano.
Vilevile amesema JATU Plc mkakati wake ni kuwaunganisha wakulima wadogo wadogo kufanya kilimo cha umwagiliaji na chenye kuleta tija kwa upande wao.
Amesema hata Serikali ya awamu ya sita inasisitiza zaidi kilimo kwa ajili ya maendeleo ya uchumi wa viwanda
Ameongeza kuwa uchumi wa viwanda unamanufaa makubwa kwa wanawake na Taifa kwa ujumla hivyo wananchi wametakiwa kulima zaidi kilimo cha mikakati .
Simbano amesema uchumi wa viwanda utakua kwa kasi kama kutakuwa na malighafi za viwanda .
Aidha amesema JATU Plc inafanya miradi ya kilimo katika mikoa ya Manyara wilayani Kiteto ambapo ina lima mahindi na alizeti, Morogoro Wilaya ya Kilosa wanalima zao la mpunga.
More Stories
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi
Mwanasiasa mkongwe afariki Dunia
Rais Samia Kuzindua Sera Mpya ya Elimu na Mafunzo