November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wanawake wametakiwa kupima mabusha

Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma.

KUELEKEA kilele cha maadhimisho ya magonjwa ambayo hayapewi kipaumbele Duniani Januari 30,2023 ,wanawake wametakiwa kujitokeza kwenda kupima kama  sehemu zao za siri zinaonesha kuvimba ili kugundua kama ni ugonjwa wa mabusha.

Wito huo umetolewa na Meneja wa Mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi vipaumbele (NTP),Dkt.George Kabona wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mpango huo unavyodhibiti magonjwa hayo.

Dkt.Kabona amesema kuwa wanawake wamekuwa waoga kujitokeza kwenda kupima wanapona sehemu zao za siri zinamabadiliko hivyo inakuwa ngumu kupewa dawa za kutibu au kudhibiti ugonjwa unapompata.

“Wanawake wengi hawataki kuja kupima hata akiona anamabadiliko hayo ila baadhi yao wanagundulika kipindi wanachokwenda kujifungua hivyo ni ngumu kumpata mwanamke mwenye ugonjwa wa mabusha na kudhibiti ugonjwa huo,”amesema Dkt.Kabona.

Dkt.Kabona amesema kuwa maadhimisho hayo yatahitimishwa Mkoani Tanga,yanayokwenda na kauli mbiu ya “Chukua hatua sasa kwa pamoja tuchukue hatua tuwekeze sasa “ambapo wanatarajia kufanya upasuaji wa mabusha kwa watu 350.

Ameeleza kuwa mpango huo umeanza 2009 ambapo amesema Tanzania kuna magonjwa 29 ambayo hayapewi kipaumbele lakini mpango huo umeanza na magonjwa matano ambayo ni Matende na mabusha 

Kichocho,Trakoma/vikope,Usubi na Minyoo ya tumbo na yanatarjiwa kumalizwa ifikapo 2030.

Aidha ameeleza jinsi watakavyoazimisha maazimisho hayo ambapo amesema watatoa huduma kutoa huduma ya oparesheni ya mabusha,kusawazisha vikope ambapo oparesheni hizo zinaendelea kambi ya Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma,Simbanjiro, Karatu Mkoani Arusha na wilaya ya Magu Mkoani Mwanza tangu kuanza kwa maadhimisho hayo Januari,2023.

Dkt.Kabona amafafanua ugonjwa wa trakoma jinsi unavyoathiri macho ambapo amesema  macho yanapata wadudu na mwanzoni  haukusumbui sana ila unavyozidi kuugua unatengeneza ukungu kwa ndani ukikaa muda unavyosugua unapata kovu.

Amesema kama usipoondolewa mapema utasugua kioo cha jicho hadi mgonjwa atapata upofu.

“Dalili za trakoma ni matongotongo macho mekundu baadae inapona ndio maana tunatoa dawa mara moja kila mwaka katika  wilaya zilizoathirika na waathirika wakubwa wakubwa wa ugonjwa huu ni watoto kuanzia miaka mitano hadi 14 na athari zake zinatokea ukifika miaka 50 pasipo kudhibitiwa,”amesema Dkt.Kabona.

Kwa upande wake Afisa wa mpango huo anayeshughulika na ugonjwa kichocho,Mohamed Nyati ameeleza kichocho kinavyompata mtu ambapo amesema kisababishwa na minyoo kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kupitia konono kwa kupitia haja ndogo au kubwa .

“Kwa tafiti tulizofanya mwaka 2004  Tanzania ,kichocho kiliathiri  Halmashairi zote  184,hasa kwenye maeneo yale ambayo wanalima mpunga ,kwenye maziwa na kwenye maeneo ambayo maji yatuama,”amesema Nyati.

Nyati amesema kuwa Halmashairi saba nchini zimeweza kutokomeza kabisa kichocho ambapo mpango huo  unampango wakutoendelea kutoa dawa za kichocho.

Naye Afisa wa mpango huo,Dkt.Clarer Jones anayeshughulika na Ugonjwa wa minyoo ya tumbo katika mpango huo amesema kuwa ugonjwa huo ni ugonjwa unaoathiri rika zote na  husababisha vitu vingi mwilini ikiwemo ukosefu wa damu, uvimbe wa tumbo na  utapiamlo.

Dkt. Clarer ameeleza kuwa Tanzania imeathiri sana watoto na ndiyo maana wao wanashughulika na kudhibiti kwa kumezesha dawa watoto wa rika la shule kuanzia miaka tano hadi 14.

Afisa wa mpango huo anayeshughulika na Ugonjwa wa matende na mabusha Oscar kaitaba,ameeleza kuwa matende na mabusha ni ugonjwa mmoja ambao unaweza kuuita  ngirimaji na unaambukizwa na mbu wa aina zote.

“Mwanzo katika utafiti kulikuwa na Halmashairi 119 ambapo 2006 tulianza kutoa dawa lakini 2009 tuliungana na kuanza kugawa dawa mara moja kwa mwaka ambazo ni mectizan na Albendazole kwa kuchanganya hizo dawa ndo tunaweza kudhibiti matende na mabusha,

“Kwakushirikiana na TAMISEMI tumeweza kutokomeza kwa halmashauri 110 hadi sasa tumebaki na Halmashairi 9 hivyo tunawasihi wananchi waweke maeneno yao safi na kulala kwenye chandarua,kuua madharaia ya mbu kulala kwenye chandarua chenye dawa,”amesema Kaitaba.