January 9, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wanawake wajasiriamali waaswa kushiriki vikundi vya umoja

Na Queen Lema, TimesMajira Online, Arusha

Wanawake wajasirimiali wa masokoni hapa nchini wameaswa kuhakikisha wanakuwa katika vikundi vya umoja ili waweze kufikiwa na fursa mbalimbali kama vile fursa za kiuchumi lakini pia hata fursa za kiteknolojia ambazo wakati mwingine hutolewa kupitia vikundi

Hayo yameelezwa jana na Jane Mgigita kutoka katika asasi ya Equalityfor Growth wakati akiongea na wajasiriamali wanawake kutoka katika soko la Kilombero ambao walitembelewa na wadau kutoka katika katika mkutano wa Asasi za kiraia(Azaki) unaendelea Arusha

Jane amesema kuwa mwanamke wa sokoni mara nyingi huwa anaamka kwake yeye kama yeye na kwa kuwa anajitafutia mwenyewe lakini ili aweze kufikiwa na fursa mbalimbali anatakiwa kuwa na wengine

“nawasihi sana wakina mama Wa sokoni hakikisheni kuwa mnakuwa wamoja hasa katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi huwezi kupata huduma iwapo upo peke yako lakini mkiwa wengi ni raisi sana kuweza kusaidia kama kikundi”ameongeza

Wakati huo huo ameishauri Serikali kuhakikisha kuwa wanaendelea kuboresha mifumo ya wanawake katika masoko ili kuweza kuwasaidia kuweza kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa

“sisi kwa kutambua hilo tuna mradi ambao tumeshautekeleza kwenye baadhi ya mikoa ila Arusha nayo ipo mbioni,tunataka kuona wanawake wa Masokoni nao wanapata haki zao za msingi ha sa kwa kuwaboreshea mazingira”ameongeza

Naye wakili Deo Bwire Kutoka katika Shirika la Legal Service Facility amesema kuwa ili wanawake wa Masokoni waweze kusaidika wanaitajika mara kwa mara waweze kuwa na Mikutano na wanasheria ambapo sasa watalamu wa sheria wataweza kuwasaidia hasa kwenye masuala yanayohusiana na haki zao za msingi

Wakili Bwire amedai kuwa wakati mwingine wajasiriamali hasa wanawake wanashindwa kupata haki Zao kwa kuwa tu Hawajui kuirafsiri sheria hasa kwa lugha ya kiswahili

Naye Diwani kata ya levolosi Agustino Matemu amesema kuwa kwa sasa wanawake hawapaswi kukaa nyuma bali wanatakiwa waweze kunyanyuka tena kwa kumuangalia Raisi wa Nchi Samia Suluhu Hasani.

Matemu amemalizia kwa kusema kuwa atahakikisha kuwa anapaza sauti za wanawake hasa pale wanapoonewa au kukandamizwa na sheria kwani wanawake kwa sasa wanachangi sana ongezeko la pato la uchumi.