
Na Israel Mwaisaka, Nkasi
Mkoa wa Rukwa umeadhimisha Siku ya Mwanamke Duniani kupitia maadhimisho yaliyoandaliwa na Plan International, yakilenga kuwawezesha wanawake na wasichana pamoja na kutambua mchango wao katika maendeleo ya jamii.
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo mwakilishi kutoka Plan International Christina Luhanda ameainisha Kupitia miradi mbalimbali, zaidi ya watoto 13,857 wananufaika na programu za elimu ya jinsia kwa vijana, mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia, pamoja na uwezeshaji wa vikundi vya vijana na wanawake kupitia mikopo na shughuli za kiuchumi.

Katika maadhimisho hayo, wanawake vinara kutoka vikundi na watu binafsi wametambuliwa na kupatiwa tuzo pamoja na vifaa vya kuwaongezea thamani katika shughuli zao za uzalishaji na biashara.
Tuzo za Wanawake vinara katika vikundi zilizotolewa zimelenga kutambua vikundi vya Wanawake vinavyoleta mabadilko chanya katika jamii, kupitia uongozi,ujasiliamali au shughuli zinazochangia maendeleo ya Wanawake na kusaidia makundi mbalimbali yenye uhitaji.
Vikundi vilivyopata tuzo ni KK Group Kristo Mfaulme Manispaa ya Sumbawanga,Villa Kizwite Vicoba Sumbawanga Manispaa na Mtu binafsi ni Imani mjimwema Nkomolo wilayani Nkasi,Aida H.Mkemwa Sumbawanga Manispaa, Neema Shambani Kifu wa Wilaya Nkasi na Tatu Said Ngaza Kalambo

Mkuu wa mkoa Rukwa Charles Makongoro Nyerere ambaye aliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya Nkasi Peter lijualikali aliwahimiza wadau wote kwa pamoja wa mkoa Rukwa kuendelea kuimarisha ulinzi wa haki za Wanawake na Wasichana pamoja na kuongeza fursa za ajira zenye staha.
Amedai kuwa bado mkoa Rukwa unashuhudia vitendo vya ukatili dhidi ya Mtoto wa kike na kuwa Wadau wote wa mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili kwa Wanawake wanalo jukumu la kuhakikisha vitendo hivyo vinatokomezwa kwa kuchukua hatua za kisheria hasa pale inapobainika kuwapo kwa vitendo hivyo popote pale

More Stories
Kamati ya Kudumu ya Bunge Nishati ya Madini yaridhishwa na maendeleo ya kiwanda cha Nguzo za Zege
Kamati ya Bunge yaridhishwa na kiwanda cha nguzo za Zege Tabora
Mhandisi Saidy: Wananchi wanayomatumaini makubwa na REA