Na Moses Ng’wat, Songwe.
MKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo, amewataka wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi Mkuu, huku akisema wanawake wanaweza.
Chongolo amesema hayo, wakati akizungumza kwenye kongamano la uzinduzi wa jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi Mkoa wa Songwe.
Amesema wanawake wanaweza kama alivyo kiongozi Mkuu wa nchi, Dkt. Samia Suluhu Hassan, hivyo kuwaasa kujiamini na kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye chaguzi zijazo.
Lakini pia Chongolo amewata wanawake hao kuhakikisha wanahuisha taarifa zao kwenye daftari la wapiga kura ili kutimiza haki yao ya kikatiba ya kuchagua na kuchaguliwa kwenye chaguzi hizo.
“Katika ngazi ya Taifa, Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM tayari ina mgombea wake wa u-Rais “Dkt. Samia” lakini kwa ngazi hizi za chini niwaombe muendelee kujiandaa na kujitokeza kugombea” amesisitiza Chongolo.
Aidha, Chongolo amewapongeza wanawake kwa kuungana na kuwa na majukwaa kwa ngazi mbalimbali ili kushauriana mambo lukuki ikiwemo kuwezeshana kiuchumi.
Mwenyekiti wa jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi Taifa,Fatuma Kange, amewataka wanawake wenzake kuendelea kuimarisha umoja katika majukwaa yao kwa ngazi zote ili kujiinua katika nyanja mbalimbali ikiwemo kiuchumi kuelekea chaguzi za baadaye 2024 & 2025.
Akifunga kongamano hilo, Katibu Tawala (RAS) Mkoa wa Songwe, Happiness Seneda, amewasihi wanawake kuendelea kujiamini na kufanya kazi kwa bidii ili kutimiza malengo yao na kuendelea kuiunga mkono Serikali katika kufikia maendeleo endelevu.
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakaniÂ
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best