January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wanawake soko la Batiki Mchikichini watoa kilio Kwa Rais Dkt. Samia

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala

Umoja Wanawake wa kutengeza batiki soko la Mchikichini wametoa kilio chao kikubwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan,wa Wanawake wa soko hilo mikopo ya Halmashauri imewapitia pembeni hivyo kupelekea kukosa mitaji ya Biashara .

Umoja wa Wanawake wa soko la Mchikichini (KIUWASO )wamesema hayo katika mafunzo iliyoandaliwà na Umoja huo wa Wanawake wa Batiki Mchikichini kwa kushirikiana na Benki ya Azania ambao walikuwa wakitoa Elimu ya mikopo.

Akizungumza katika mafunzo hayo Katibu wa Wanawake wa soko la Mchikichini Adela Raymond Swai, amesema umoja wanawake wa Batiki wa soko la Mchikichini mikopo ya Serikali imewapitia nyuma hivyo ulazimika kutafuta njia ya ziada waweze kupata mitaji.

“Tunaomba Serikali yetu sikivu inayoongozwa na Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan isikie kilio chetu Umoja wanawake wa Batiki wa soko la Mchikichini tuwezeshwe mikopo ya Serikali tuweze kukuza mitaji yetu ya biashara katika soko letu tumekuwa tukifatilia mikopo ya Halmashauri bila mafanikio ” amesema Adela.

Adela amesema Batiki zote utakaziona ,Kenya ,Uganda ,na nchi za Afrika zote zinazalishwa na Umoja wanawake wa Mchikichini Wilayani Ilala.

Makamu Mwenyekiti wa Umoja wanawake Mchikichini Elnaike Kimati amesema changamoto kubwa katika umoja wao vitendea kazi wanatumia moto wakati wote wanaomba serikali iwatazame kwa jicho la Karibu ,ambapo toka soko hilo liungue wameathitika ukosefu wa mitaji pamoja na Bima wengi hawana wakiunguliwa wanajenga wenyewe kwa pesa zao.

Makamu Mwenyekiti Kimati ameiomba Serikali kupitia Waziri wa Biashara kuwatafutia fursa na masoko ya nje Ili waweze kukitangaza zaidi pamoja na nchi yetu .