
Na Israel Mwaisaka, Nkasi
Kuelekea maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani jumuia ya kikristo Tanzania (CCT) idara ya Wanawake imefanya kongamano kubwa ambalo limewakumbusha wajibu wao na kutambua haki zao ikiwa ni pamoja na kumtanguliza Mungu kwa Kila jambo.
Akitoa mahubiri kwenye kongamano hilo lililofanyika katika kanisa la Anglikana mjini Namanyere mhubiri Debora Kaguo alidai kuwa Mwanamke ndiyo nguzo kuu katika malezi ya familia hivyo anatakiwa kuwa ni Mtu anayejitambua na kujua anachokifanya.

Amesema kuwa ndoa kwa kiasi kikubwa inajengwa na Mwanamke na kuwa ni jukumu la Mwanamke kumlinda Mumewe lakini si kwa kukagua simu akiwa amelala au kumfuata Kila aendako na kwenda kuanzisha ugomvi na Wanawake wengine Wenye mahusiano na Mume wako Bali ni kumhudumia vyema na kumuombea mbele ya Mwenyezi Mungu
Mhubiri Kaguo amesema kuwa kwa Sasa ndoa nyingi ni za moto hivyo ni muhimu kwa Sasa wakautumia muda mwingi kuzirekebisha ndoa zao badala ya kuutumia muda mwingi kuzungumza mambo yasiyokuwa na msingi Wala tija kwao

Mgeni rasmi katika kongamano hilo ambaye ni afisa elimu msingi Eliud Njogela ambaye aliwakilishwa na Noel Kiombo aliwakumbusha Wanawake kuendelea kulinda heshima ya Mwanamke kwa kuwa wanyenyekevu na wenye kuwajibika ipasavyo katika majukumu yao


More Stories
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi
Waziri Mkuu kuanza ziara mkoani Rukwa Marchi 8 Hadi 10