January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wanawake 100,000 wampa tano Rais Samia kwa kuongeza asilimia 23.3 ya mshahara

Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online

Na Mwandishi wetu Timesmajira online

TAASISI isiyokuwa ya kiserikali inayowauganisha Wanawake Nchini kwa kupinga ukatili na kuwawezeha kiuchumi Wanawake 100,000 imesema wamefurahishwa na hatua ya serikali kuongeza mshahara kwa asilimia 23.3 hali itakayoleta unafuu wa maisha.

Hayo yamebainishwa Jijini Dar es salaam leo na Mkurungezi Taifa wa haki za wanawake kutoka taasisi wanawake 100,000 Josephine Matiro wakati wakimpogeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuhusu ujasiri wa kipekee.

Matiro amesema hatua ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,Rais Samia Suluhu Hassani,kuongeza mshahara kwa mara kwanza toka miaka saba ipite kimekuwa faraja kwa watanzania na pia kimewatia moyo watumishi wa umma ambao kwa kipindi kirefu ambao walikuwa hawajaongezewa mshahara.

“Ongezeko hili la mshahara ni kubwa kuwahi kutokea nchini kwa kipindi kirefu sana kwa miaka mingi sasa , wafanyakazi nchini wamekuwa na kilio cha kutoongezwa mshahara na kutokupandisha vyeo kwa watumishi wa umma”amesema Matiro

Na kuongeza kuwa” ndani ya miaka mingine mmoja tu Rais Samia ameweza kuongeza mshahara kwa asilimia 23.3 amepandisha watumishi wa umma Maharaja na kulipa malimbikizo ya mchango wa pensheni za watumishi”aliongeza

Aidha,kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake 100,000 Vicky kamata amempongeza Rais Samia katika kuonesha jitihada za kupambana na kupanda kwa bei ya mafuta duniani kwa kutoa shilingi bilioni mia moja na kusema hatua hiyo itapelekea kuleta nafuu kwa watanzania.

“Kiasi hiki cha ruzuku kukabiliana na ongezeko la bei ya mafuta Duniani hakijawahi kutolewa na serikali ya Tanzania tangu ipate Uhuru lakini kwa ujasiri wa kipekee “amesema kamata

Naye Mkurugenzi wa Miradi wa Taasisi wanawake laki moja,Nangasu Warema,amesema Taifa linatarajia kupata manufaa makubwa kutokana na ujio wa Filamu ya Royal Tour kwenye upande wa utalii na kumpongeza Rais Samia kuja ubunifu huo.

Amesema Filamu ya Royal Tour ni Ubunifu na jitihada kubwa za kutangaza fursa za utalii na uwekezaji nchini ambazo hazijawahi kutokea tangu Uhuru takribani miaka 60 iliyopita.

“Kupitia ushiriki wake kwenye Royal Tour Rais Samia amewesha kuitangaza Tanzania kimataifa na kupeperusha bendera ya nchi”amesema Werema

Balozi wa Utalii Tanzania na Mkurugenzi wa Miradi, Wanawake 100,000 Nangasu Warema akizungumza na waandishi wa habari kulia kwake ni Mkurungezi Taifa wa Haki za wanawake 100,000 Josephine Matiro na Mwenyekiti wa wanawake 100,000 Vicky Kamata wakizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam mapema Leo hii