Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema litaendelea kuimarisha ulinzi wa Mkoa huo ambao ndio kitovu cha utalii hapa nchini huku likibanisha kuwa limeendelea kutoa elimu kwa madereva wanao pokea na kutoa huduma ya usafiri kwa wageni wanafika Mkoani humo kwa ajili kutalii.
Akiongea mara baada ya kikao hicho kikichohusisha wadau wa usafirishaji wa Utalii Mkuu wa Opersheni za Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Salvatory Makweli amesema kuwa huo ni mwendelezo wa kutoa Elimu na kuweka mazingira bora na salama kwa wageni wanaokuja kutalii Mkaoni humo kwa ajili ya kitalii.
ACP Makweli amewetaka Madereva hao kutambua kuwa kipindi hiki ndicho watalii wengi wanafika katika Mkoa huo kwa ajili ya kutalii ambapo amewataka wasafirishaji hao kuweka utambuzi wa vyombo vyao ili kuwabaini wanaochafua taswira nzuri ya watoa huduma hao kwa wasafiri kwa watalii.
Amewetaka kutambua endapo watatekeleza agizo hilo watakuwa wamepunguza na kuondoa malalamiko ya wageni ambao wamekuwa wakilalamika juu ya watoa hudma hao katika jiji la Arusha.
Kwa upande wake Alex Athony ambaye ni mdau wa usafirishaji watalii licha ya kushukuru kwa elimu hiyo amebainisha elimu walio ipata itaongeza chachu ya huduma bora kwa watalii huku akiweka Wazi kuwa licha kutoa huduma hiyo magari wanayotumia ni magari ambayo yanakizi viwango kwa vya kutoa huduma kwa wageni na watalii.
Nae Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani Mkao wa Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Zauda Mohamed amesema kuwa kikosi hicho kimeendela kutoa elimu ili kuweka mazingira salama kwa watalii wanaofika Mkoani humo kwa ajili ya utalii huku akiwataka kuwa mabalozi wazuri ambao wataitagaza Arusha na Tanzania kwa ujumla.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua