Na Esther Macha, Timesmajira Online , Mbeya
WANA Ndoa wawili wakazi wa mtaa wa TEKU Viwandani mkoani Mbeya wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kumuua kwa kumpiga na fimbo sehemu mbalimbali za mwili mtoto wao Chloy Ramadan (4) kwa kosa la kujisaidia kwenye nguo.
Akizungumzia tukio hilo Novemba 26,2024 Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya , Benjamin Kuzaga amesema kuwa tukio hilo limetokea Majira ya saa 2.00 usiku Novemba 25,mwaka huu katika mtaa wa TEKU Viwandani Jijini hapa.
Kuzaga amewataka Wana ndoa hao kuwa ni Ramsadhan Mwakilasa(28)Mariam Mwashambwa(28)ambao walishirikiana na mama wa kambo wa mtoto huyo kumpiga na fimbo Mtoto huyo sehemu mbalimbali za mwili wake .
Hata hivyo Kamanda kuzaga amesema uchunguzi wa tukio hilo umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni ukatili na unyanyasaji kwa kumuadhibu mtoto baada ya kujisaidia kwenye nguo alizokuwa amezivaa.
Jeshi la Polisi linawataka wazazi/walezi kuacha vitendo vya kujichukulia sheria mkononi dhidi ya watoto pindi wanapokosea na badala yake watumie njia sahihi na salama kuwafundisha au kuwaelekeza bila kusababisha madhara.
More Stories
Watoto wenye uhitaji wapatiwa vifaa vya shule
Wananchi Kisondela waishukuru serikali ujenzi shule ya ufundi ya Amali
RC.Makongoro ataka miradi itekelezwe kwa viwango