Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
WITO umetolewa kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam, kuwekeza katika kilimo cha Vanilla, kutokana na tija ya kuwaendeleza kiuchumi, kwani inafaida kubwa na inastawi vizuri katika Mkoa huo.
Wito huo, umetolewa jijini Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanila International Limited, Simon Mnkondya wakati akikagua mashamba yake ya Vanila yaliyopo Mkoa huo.
Alisema kilimo cha Vanila kina tija kubwa ya kuwakwamua wananchi kiuchumi kama wataamua kuwekeza kwani hakitumii muda mrefu kulima hadi kuvuna.
“Bado Watanzania wengi hawaja fahamu siri hii ya kilimo cha Vanila, lakini tunaendelea kutoa elimu wajue utajiri uliojificha katika uwekezaji huu wa Vanila, kwani wale waliodhubutu wameona faida zake, hivyo naendelea kuwahamasisha na kutoa elimu kwa Kwa jamii juu ya kilimo hiki, wasipotezw muda kwa kuwekeza mazao yenye hasara,”alisema Mnkondya.
Akielezea mashamba yake, yaliyopo Mkoa wa Dar es Saam aliyataja kuwa ni Kunduchi na Ununio, Ubungo, Msewe na Boko Calfonia ambapovanila imestawi vizuri kwa zaidi ya mita 12 kwa rando(tawi), yanasababisha mkulima kupata pesa nyingi sana kwa maana marando ya vanilla ni biashara isiyokuwa na Mipaka.
Pia, alisema anao uwekezaji mkubwa uliopo katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Njombe, Dodoma, Kagera, Mwanza na mikoa mingineyo ambako anavuna utajiri wa fedha, hivyo wananchi wajitokeze kuwekeza Kwa maendeleo yao.
Aidha, Mkurugenzi Mkondya, aliishukuru serikali kwa kuendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji wa kilimo cha Vanila nchini, jambo ambalo linafungua fursa zaidi kwa Watanzania wa ndani na nje ya nchi.
More Stories
‘Ni Wasira ‘Makamu Mwenyekiti CCM Bara
15 mbaroni tuhuma wizi wa shehena ya unga wa sembe
Wacheza rafu Uchaguzi Mkuu ujao waonywa