December 28, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wananchi wanaozunguka mgodi wa Bulyanhulu wanufaika na miradi

Na Judith Ferdinand,TimesMajira online,Mwanza

WANANCHI 50,000, wanaozunguka Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu, Kata ya Bulyanhulu Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga wamenufaika na miradi mbalimbali ikiwemo ya maji,afya,elimu pamoja na huduma ya mradi wa makundi maalumu.

Miradi hiyo imetekelezwa na mgodi huo,kupitia uwajibikaji wa mgodi huo wa Bulyanhulu kwa Jamii (CSR) kwa mujibu wa sheria ya madini.

Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu, Mary Lupamba(kushoto) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri,Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi,Vijana, Ajira na Walemavu, Patrobas Katambi(wa kwanza kulia) alipotembelea banda la mgodi huo kwenye maonesho ya Usalama na Afya mahali pa Kazi,yanafanyika jijini Mwanza kuelekea siku ya usalama na afya duniani yanayofanyika uwanja wa Nyamagana mkoani hapa kuanzia Aprili 26 hadi Mei Mosi mwaka huu.picha na Judith Ferdinand

Hayo yamebainishwa na Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu,Mary Lupamba, wakati akitoa maelezo kwa Naibu Waziri,Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi,Vijana, Ajira na Walemavu, Patrobas Katambi, alipotembelea banda la mgodi huo kwenye maonesho ya Usalama na Afya mahali pa Kazi,yanafanyika jijini Mwanza kuelekea siku ya usalama na afya duniani yanayofanyika kuanzia Aprili 26 hadi Mei Mosi mwaka huu.

Lupamba,amesema uwajibikaji wa mgodi kwa jamii,mgodi huo umefanikiwa kutekelea miradi mbalimbali inayowanufaisha wananchi wanaouzunguka ambapo Kituo cha Afya cha Bugarama ni moja ya miradi ya ujenzi uliotekelezwa katika sekta ya afya huku mingine iliyotekelezwa kwenye sekta hiyo ni pamoja na zahanati za vijiji 10 wilayani Nyang’hwale na zahanati ya Kijiji cha Kakola Msalala.

Amesema,katika sekta ya elimu kila mwaka mgodi kwa kushirikiana na serikali ulitekeleza miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule mbalinbali za msingi ,maabara,mabweni na samani katika shule za sekondari za halmashauri za Msalala na Nyang’hwale,pia wamekuwa na mradi wa kuboresha ufaulu wa kidato cha nne wilayani Nyang’hwale.

Baadhi ya wafanyakazi wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu wakiwa kwenye banda la mgodi huo kwenye maonesho ya Usalama na Afya mahali pa Kazi,yanafanyika jijini Mwanza kuelekea siku ya usalama na afya duniani yanayofanyika uwanja wa Nyamagana mkoani hapa kuanzia Aprili 26 hadi Mei Mosi mwaka huu.Picha na Judith Ferdinand

Pia,katika sekta ya maji mgodi huo unashirikiana na serikali kutekelea mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria utakaonufaisha wananchi 100,000, katika Wilaya za Kahama na Nyang’hwale ambapo Mgodi wa Bulyanhulu unafanya kazi na kamati za maendeleo katika halmashauri za Msalala na Nyang’hwale kupanga ,kutekelea na kuratibu mipango ya kila mwaka ya uwajibikji wa mgodi katika jamii.

Sanjari na hayo amesema,huduma kwa makundi maalum kwenye jamii ambapo baadhi ya wanufaika wa fedha za uwajibikaji kwenye jamii ni pamoja na wazee kupitia mradi wa bima ya afya kwa wazee zaidi ya 60 katika vijiji jirani na mgodi huo.