Na Mwandishi Wetu, Timesmajiraonline,Dodoma
WANANCHI wamezidi kumiminika kwa wingi katika Banda la Mama Samia Legal Aid Campaign ili kupata msaada wa kisheria, jijini Dodoma, huku ikiwa imebakia siku moja kumalizika kwa Maonesho ya Wakulima na Wavuvi Nanenane.
Maonesho hayo yamekuwa fursa muhimu ya kutoa elimu mbalimbali kwa wakulima na wavuvi, yamekuwa kivutio kikubwa kwa jamii, huku huduma za kisheria zikitolewa kuwasaidia wananchi kutatua changamoto zao za kisheria na kupata haki zao.
Kupitia maonesho hayo yenye kauli mbiu “Chagua Viongozi Bora wa
Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”, ambapo wabobezi katika tasnia hiyo ya sheria wametumia fursa hiyo kutatua migogoro mbalimbali
inayotokea kwenye jamii katika mkoa wa Dodoma na maeneo mbalimbali
wanakopita.
“Nimefurahi sana kuwepo kwa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia imekuwa msaada mkubwa kwa wananchi napendekeza kama itampendeza Rais Samia hii isiwe tu kampeni maana kampeni inaisha muda ila ikiwa Taasisi ya kudumu itawasaidia sana wananchi wanyonge ambao wanapambana sana kusaka haki zao kisheria,” alisema.
Mkazi wa Area C Dodoma, Thomas, alisema katika maonesho ya nanenane
amejifunza kupitia kampeni hiyo itasaidia wananchi wengi wasiokuwa na
uelewa wa kisheria kuhusu masuala mbalimbali.
More Stories
Premier Bet yamtangaza mshindi mkubwa
Dkt. Kazungu atembelea miradi ya umeme Dar es Salaam
MSF ilivyojidhatiti kusaidia serikali katika utoaji wa huduma za afya