December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wananchi waishio eneo la hifadhi Ngorongoro kuhamia makazi mapya

Na Hadija Bagasha, TimesMajira Online, Tanga

Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana amesema kuwa wakati wowote kuanzia sasa wananchi waishio katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro wataanza kuhamia katika makazi mapya yaliyopo Kijiji cha Msomera kilichopo Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga baada ya serikali kujiridhisha maandilizi mengi yamekamilika.

Pia Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt Pindi Chana Amesema Kuwa Baada ya Nyumba 100 kujengwa katika Kijiji hicho cha Wilayani Handeni Serikali iko Mbioni Kujenga nyumba zingine 400 Mahala hapo.

Balozi Dkt. Chana ametoa kauli hiyo mara baada ya kufanya ziara ya kukagua hali ya utayari wa miundombinu ya makazi, maji, umeme, madarasa ya shule za msingi na sekondari, zahanati, majosho kwa ajili ya mifugo, na barabara katika Kijiji hicho.

“Kuanzia sasa wakati wowote kaya hizi zitakuwa zinaingia hapa Handeni Msomera tumeangalia na kujiridhisha kwamba maandalizi mengi makubwa yamefanyika ikiwa ni pamoja na shule za msingi za sekondari muda wowote kuanzia sasa wanangorongoro waliojiandikisha kwa hiari watahamia hapa kuendelea na maisha ili kupisha shughuli za Uhifadhi ndani ya eneo”, “alisistiza Balozi Waziri Chana.

“Nimekuja Leo hapa Msomera Kujionea Maandalizi Haya Kiukweli Nasema nimeridhika Sana Timu ya Maandalizi Haya imefanya Kazi kubwa na ni Nzuri mnoo” Alisema Waziri Chana.

Dkt Chana Amesema kwamba tayari Serikali Kupitia Wizara yake inamalizia Utaratibu wa Mwisho wa Kuanza kuwaleta Wakazi Wanaotoka kwa hiyari yao katika Hifadhi ya Ngorongoro kwenda katika Kijiji hicho.

“Miundombinu ya Nyumba za Makazi,Shule ,Kituo Cha Afya,Umeme, Maji, Barabara Sanjari na Majosho ya Mifugo yote hiyo imekamilika na Muda Wowote kutoka Sasa Wananchi hao Watafikishwa kwenye kijiji hiko kwaajili ya Makazi Yao Mapya.

Ameeleza kuwa pamoja na kukamilika kwa ujenzi wa nyumba 103 na huduma zingine za kijamii, Serikali inajipanga kuanza awamu ya pili ya ujenzi wa nyumba za makazi 400 kwa ajili ya kuwezesha wananchi wanaoendelea kujiandikisha kwa hiari kuhamia Msomera.

Aidha,Waziri Huyo Wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt Pindi Chana Amemaliza Kusema Kuwa Suala la Serikali ya awamu ya Sita kuwahamishia Msomera Wakazi Wa Hifadhi ya Ngorongoro ni Jambo la Kupongezwa na ni la kiuungwana Sana kwakuwa linalenga kuifanya Hifadhi ya Ngorongoro kulindwa kwaajili ya Uhifadhi na hatimae Serikali kuingiza Mapato Kupitia Utalii.

Kwa upande wake Mkuu Wa Mkoa Wa Tanga Adam Kigoma Malima amemshukuru Waziri huyo kwa Kufanya ziara katika Kijiji hicho na huku akiongoze kusema kwamba Viongozi wa Mkoa Wa Tanga Wakishirikiana na Viongozi Wa Mkoa Wa Arusha, Viongozi Wa hifadhi ya Ngorongoro sehemu ambayo wanapokea wakazi hao kwa pamoja wako tayari kulisimamia Kikamilivu zoezi la kuwapokea kwenye kijiji hiko Cha Msomera.

Malima ameleeza kuwa mkoa huo umeshaandaa mazingira ya kuwapokea wananchi wa Ngorongoro na hali ya kiusalama iko shwari na tayari vyumba saba vya madarasa, Maabara, Bweni na majosho kwa ajili ya mifugo yamekamilika sambamba na usambazaji wa huduma za maji, umeme na mawasiliano ya barabara.

Akiwa katika ziara ya Mhe Waziri, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongela ameeleza kuwa uongozi wa mkoa wa Arusha kuratibu zoezi la kuandikisha wananchi wanaotaka kuhama kwa hiyari na kaya zilizokwisha jiandikisha Serikali imeshapanga utaratibu wa kuwahamisha muda wowote kuanzia sasa