November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wananchi wafurahishwa na huduma ya PSSSF kiganjani Mobile App

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

WANACHAMA wengi wa PSSSF waliotembelea banda la Mfuko huo kwenye Maonesho ya Wiki ya Sheria kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, wamefurahishwa na huduma ya PSSSF Kiganjani Mobile App.

Huduma ya PSSSF Kiganjani Mobile App, inamuwezesha mwanachama kupata taarifa zote zinazohusiana na uanachama wake akiwa mahali popote kupitia simu yake ya kiganjani, Mtaalamu wa Mifumo ya Kompyuta wa Mfuko huo Bw.Gideon Mwashihongo amesema leo Januari 28, 2024, wakati akitoa elimu ya matumizi ya huduma mtandao.

Bw. Kizza Sostenes, Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba, Wilaya ya Temeke, ameupongeza Mfuko huo kwa kutoa huduma zake kidijitali.

“Nimefaidika sana baada ya kufika hapa, nimeelekezwa jinsi ya kutumia huduma ya PSSSF Kiganjani na nimeijaribu ni huduma nzuri na rahisi kutumia.” Amesema Bw. Sostenes.

Mwanachama mwingine Bi. Lightness G. Msuya, yeye amesema huduma ya PSSSF Kiganjani Mobile App, inasaidia kuokoa muda, kwani yeye kama mtumishi, inamsaidia kupata taarifa za Mfuko akiwa mahali popote.

Kwangu mimi huduma hii inanipunguzia gharama za usafiri kufuata huduma kwenye ofisi za PSSSF, kuanzia sasa silazimiki kwenda PSSSF, baada ya kujiunga kwenye huduma hii, kwani simu yangu inatosha.” Amesema Mwnachama mwingine wa PSSSF, Bw. Kudura Said Kondo, mtumishi wa Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia ushiriki wa Mfuko kwenye maonesho hayo, Bw. Kikula Suleiman, kutoka Kurugenzi ya Huduma za Sheria PSSSF Makao Makuu amesema, PSSSF kama taasisi iliyoundwa kisheria ni mdau mkubwa wa Mahakama na watumishi wa mahakama na taasisi nyingine za umma ni wanachama wa Mfuko huo, hivyo ushiriki wa Mfuko kwenye Maonesho ni fursa nzuri ya kutoa huduma na elimu kwa wanachama.

“Katika jitihada za kuhakikisha wanachama wanapata huduma bora na rafiki tumeamua kujikita kutoa elimu ya huduma za PSSSF kiganjani Mobile App,  PSSSF ulipo Mtandaoni Member Portal.” Amesema na kuongeza, kwa kutumia huduma hiyo tunaamini inatoa uhuru sio tu kwa wanachama lakini pia kwa waajiri kuweza kulipia michango na kujihudumia wenyewe, yaani self-service.” Amefafanua Bw. Suleiman.

Maonesho hayo ya siku saba yaliyobeba kauli mbiu “Umuhimu wa Dhana ya Haki kwa Ustawi wa Taifa: Nafasi ya Mahakama na Wadau katika Kuboresha Mfumo Jumuishi wa Haki Jinai” yamezinduliwa rasmi Januari 27 2024, na yatafikia kilele Januari 30, 2024.

Mtaalamu wa Mifumo ya Kompyuta Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Gideon Mwashihongo (katikati), akitoa elimu ya matumizi ya PSSSF Kiganjani Mobile App, kwa wanachama wa PSSSF waliotembelea banda la Mfuko huo kwenye Maonesho ya Wiki ya Sheria viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kupitia PSSSF Kiganjani mwanachama anaweza kupata huduma zote zitolewazo na Mfuko bila kulazimika kufika ofisi za PSSS

Bw. Kikula Suleiman (aliyesimama), kutoka Kurugenzi ya Huduma za Sheria PSSSF Makao Makuu, akitoa elimu ya matumizi ya PSSSF Kiganjani Mobile App, kwenye banda la Ofisi ya Taifa ya Mwendesha Mashtaka Kanda ya Dar es Salaam kwenye maonesho ya Wiki ya Sheria, viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Januari 28, 2024.

Mtaalamu wa Mifumo ya Kompyuta Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Gideon Mwashihongo (kulia), akitoa elimu ya matumizi ya PSSSF Kiganjani Mobile App, kwa mwanachama wa PSSSF, Bi. Lihhtness G. Msuya, kwenye banda la PSSSF, Januari 28, 2024.

Mtaalamu wa Mifumo ya Kompyuta Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Gideon Mwashihongo (kulia), akitoa elimu ya matumizi ya PSSSF Kiganjani Mobile App, kwa mwanachama wa PSSSF, Bw. Kudura Said Kondo kwenye banda la PSSSF, Januari 28, 2024.

Bw. Kizza Sostenes (kulia), Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba, Wilaya ya Temeke, akihudumiwa na Bi. Hellen Mollel, Afisa Mafao PSSSF.