Na Mwandishi wetu, Zanzibar
Wananchi kutoka maeneo mbalimbali Zanzibar, wamefurahishwa na elimu ya hali ya hewa inayotolewa katika maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, yanayofanyika katika viwanja vya Maonesho ya Biashara, Nyamanzi, Mjini Magharibi, Zanzibar kuanzia Tarehe 07 – 19 Januari, 2024.
Wageni mbalimbali waliweza kutembelea banda la TMA wakiwemo viongozi wa Taasis kutoka Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Prof. Ulingeta Mbamba, Shirika la Reli Tanzania Bw. Masanja Kadogosa, Mkurugenzi wa Huduma za Taasis kutoka Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Hamidu Mbegu, Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Teophoy Mbilinyi ambao waliipongeza TMA kwa huduma nzuri ya usahihi wa Utabiri inayotolewa .
Aidha, wataalam wa hali ya hewa kutoka TMA wameendelea kutoa elimu kwa wadau mbalimbali ili kutumia huduma mahususi zinazotolewa na TMA pamoja na kuelewa namna ya kutumia taarifa za hali ya hewa kwa usahihi ili kukabiliana na athari zitokanazo na hali mbaya ya hewa.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua