Na Joyce Kasiki,timesmajira online,Ruangwa
JESHI la Zimamoto na Uokoaji limewataka wananchi kuwa na vifaa vya kuzimia moto wa awali ili kuokoa maisha ya watu pamoja na kuzuia uharibifu mkubwa wa mali zao hata kabla Jeshi hilo halijafika katika eneo la tukio.
Hayo yamesemwa na Stafu Sajenti Enock Mapunda kutoka Jeshi la Zimamoto na Ukoaji mkoa wa Lindi wakati wa maonyesho ya Madini yanayoendelea mkoani humo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa.
“Lengo la kukabiliana na moto wa awali ni kusaidia Jeshi la Zimamoto na Ukoaji kuuzima moto na pia kusaidia mali na maisha ya wananchi kuwa katika hali ya usalama kabla Jeshi la Zimamoto na Uokoaji halijafika eneo la tukio.”amesema Mapunda
Aidha amesema,Jeshi hilo limejipanga kutoa elimu kwa jamii hususan wachimba madini jinsi ya kuweza kuwa salama wanapofanya kazi yao ya kuchimba madini.
Pia amewashauri wachmba madini kuhakikisha kwamba wanapokuwa katika maduara ya uchimbaji madini wahakikishe kwamba wale wachimbaji wanaoingia pale ni wale wenye ufahamu na shughuli nzima ya uchimaji wa madini kwa siyo kila mtu anaingia kwa sababu tu ni shughuli ya kuwapatoa kipato.
Aidha amewashauri wawekezaji kufika Jeshi la Zimamoto pindi wanapotaka kufanya uwekezaji wao kwa ajii ya ushauri na kupewa na maelekezo yanayohusiana na uchimbajiwa madini.
Mbali na shughuli za uchimbaji wa madini mkoa wa Lindi una fursa nyingi katika shughuli za uwekezaji hasa uwekezaji wa Gesi Asilia .
“Katika eneo hili kuna viashiria vingi vya moto ,lakini Jeshi letu limejipanga kutoa elimu kwa jamii ambayo itakuwa karibu na maeneo ya uchumbaji wa gesi jinsi ya kuishi salama katia maeneo hayo na namna ya kukabiliana na majanga ya moto yanayoweza kutokea .”amesema Mapunda na kuongeza kuwa
“Moja ya eneo ambalo tualielekeza sana kwa jamii ni kwamba waepuke uchomaji wa moto hovyo katika maeneo yao,kama tunavyojua watu wengi wa mikoa ya Lindi na Mtwara wengi ni wakulima wa mazao ya kibiashara kama korosho ufuta na mazao mengine,
“Sasa kumekuwa na desturi ya kuandaa mashamba kwa kuchoma moto ,lakini pia kumekuwa na desturi ya watu wengi kukata misitu na kuchimba bila kujua ni wapi na kumepita nini.”
Kuifuatia hali hiyo amewashauri wananchi waishio mikoa ya Lindi na Mtwara kuwa makini na zile zinapitisha gesi na kwamba wajue njia zinazopitisha gesi na kujua jinsi gani wanaweza kuishi bila kuleta athari wala uharibifu wowote utakaopelekea uvujaji wa gesi.
Amewaasa wananchi kutemebelea viwanja vya maonyesho hasa katika banda la Zimamoto na Ukoaji ili waweze kupata elimu inayohusiana na masula ya moto pamoja na maukozi.
More Stories
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa
NLD kipo tayari kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa