December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wananchi wa  mikoa ya Nyanda za Juu Kusini tembeleeni kwenye banda la TPHPA kupata elimu sahihi  ya viuatilifu

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Mbeya

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania Prof Joseph Ndunguru amewataka wananchi wa nyanda za juu kusini kutembelea katika banda la Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania katika maonesho ya sherehe za wakulima nane nane ambayo kitaifa yanafanyika katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

Prof.Ndunguru ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda hilo huku akisema wanancghi wanaofika katika banda hilo watapata elimu ya jinsi Mamlaka hiyo inavyotumia teknolojia kubaini visumbufu vya mimea na kuvidhibiti na hivyo kuleta usalama wa chakula.

K wa mujibu wa Prof Ndunguru TPHPA imejipanga katika maonesho hayo kutoa elimu ya matumizi sahihi na salama ya viuatilifu ,vinyunyizi,udhibiti wa visumbufu vya Mimea,taratibu za uingizaji wa mazao nchini na utoaji wa mazao nje ya nchi,usimamizi wa biashara ya viuatilifu (taratibu za usajili wa Viuatilifu na biashara za viatulifu 

Pia ameeleza kuwa Mamlaka hiyo inatoa elimu juu ya uifadhi wa bioanuai za mimea, udhibiti wa visumbufu vya mimea kwa kutumia njia za kibaolojia, na udhibiti wa wa visumbufu vya mlipuko.

Mwenyekiti wa kamati ya mandalizi ya maonesho ya nane nane 2023 kwa upande wa Mamlaka hiyo Dkt Mujuni kabululu amewaomba wananchi wote kuendelea kutembelea banda la mamlaka ambapo watapafa fursa ya kukutana na wataalumu ambao watajibu maswali yote na kutoa elimu stahiki pamoja na kupokea changamoto mbali mbali za wakulima