December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wananchi Mkunduge wahimizwa kujiandikisha upigaji kura kipindi cha uchaguzi

Na Bakari Lulela,Timesmajira

UMOJA wa vijana wa chama cha mapindizi (UVCCM)wilaya ya kinondoni, jijini Dar es salaam umewataka wananchi wa mkunduge kujitokeza katika zoezi la kujiandikisha Ili kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika Oktoba 2024.

Akizungumza jijini kwenye mkutano maalum ulifanyika katika viwanja vya Cameroon mwenyekiti wa wilaya ya kinondoni Abdullahman Kassim ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo amesema Kuna kila sababu za kushiriki kwenye zoezi hilo kwa kumchagua kiongozi mchapa kazi sio bora kiongozi ambapo wanachama na makada wa chama hicho walihudhuria kwa wingi kusikiliza sera mbalimbali zinazotolewa pia viongozi wa chama wilaya, kata walishiriki kwenye mkutano huo.

“Nawapongeza wananchi wote wa eneo hili pia naomba mjitokeze kwa wingi kwenye kujiandikisha Ili kuweza kumchagua chama cha mapindizi CCM kutoka na sera ZETU mzuri kikubwa tumuunge mkono Raisi wetu jemedari Samia Suluhu Hassan,” amesema

Aidha mwenyekiti huyo amewataka wanamkunduge kutobeza sera za chama ambapo wanatakiwa kujitokeza katika zoezi Zima la kujiandikisha, kugombea uongozi na kutumia kalamu zao kwenye upigaji wa kura kwa viongozi wa CCM.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM kata ya mkunduge amewataka wanachama wa chama cha mapindizi CCM kutobagua utu wa mtu ilimradi awe timamu katika kusaidia wananchi na Taifa kwa ujumla.Hata kiongozi huyo amesema kutokana jitihada mbalimbali za uboreshaji miundo mbinu na huduma safi za maji na umeme wa kutosha unaopelekea wananchi kulidhia na ubora huo CCM Haina budi kuchukua Tena.