December 28, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wananchi Jimbo la Mbalali,kata sita wapiga kura leo

Na Mwandishi wetu, timesmajira

Wananachi wa Jimbo la Mbalali wamejitokeza kwa wingi kwenye vituo vya kupiga kura kwaajili ya kushiriki uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo hilo na udiwani wa Kata sita za Tanzania Bara ambao unafanyika leo.

Takribani wapigakura 216,282 walioandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura wanapiga kura leo.

Ambapo uchaguzi utahusisha vituo 580 vya kupiga kura na uchaguzi huo unaendelea kwa amani na utulivu katika maeneo hayo.