Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma
WADAU na Wanahisa wa Benki ya Ushirika Kilimanjaro(KCBL) kukutana kesho jijini Dodoma katika mkutano Mkuu wa 27 wenye lengo la kuwapa taarifa ya utendaji na mafanikio ya benki hiyo kwa mwaka uliopita na mipango ya mwaka ujao wanahisa hao.
Akizunguza na waandishi wa habari jijiji hapa leo,Julai 25,2024 kuelekea mkutano huo,Mwenyekiti wa KCBL Prof.Gervans Machimu amesema mkutano huo unafanyika kwa mara ya Kwanza Dodoma na ni Mkutano wa kihistoria kwa sababu utakuwa mkutano wa mwisho wa Benki ya KCBL kwani wapo mbioni kuanzisha Benki ya Ushirika Tanzania ambayo Makao makuu yake yatakuwa Dodoma.
Hivyo amesema kuwa mkutano huo utawapa fursa wanahisa kupata taarifa ya kazi ambazo zimezifanywa walizowatuma Benki hiyo,pamoja na kufahamu matarajio ya mwaka unaofuata.
“Nawakaribisha wanahisa wote kushiriki katika mkutano huu wa maendeleo ya ushirika kwani katika mkutano huu pia tutapokea taarifa ya utekelezaji kwa wanahisa na wanaushirika katika kuleta ujumuishi kwa inafanyakazi na watu kawaida kama mama ntilie na wauza nyanya,”amesema Prof.Machimu.
Kwa upande wake Meneja Mkuu wa KCBL Godfrey Ng’urah amesema kuwa pamoja na mkutano huo kutoa taarifa ya utendaji ya mwaka 2023 pamoja na safari ya miaka mitatu yakuifanya KCBL kuwa benki ya Kitaifa kutakuwa na agenda zingine katika mkutano huo.
Ng’urah ametaja agenda hizo kuwa ni pamoja na Matokeo ya kiutendaji wa biashara na huduma za kifedha.
Aidha agenda nyingine ni Mifumo ya utawala bora na tija ambayo imetokana na shughuli za utendaji.
Pia maazimio ya miaka mitatu iliyopita ya kuhamishia makao makuu Dodoma na Kilimanjaro na Tandahimba kuwa na matawi ya benki hiyo.
“Tumeshapata Ofisi Dodoma na hadi kufikia mwezi wa tisa mwaka huu tutakuwa tayari tunabenki ya ushirika Dodoma,”amesema Ng’urah.
Pamoja na hayo Ng’urah amesema kuwa mkutano huo uanatarajiwa kufuatiliwa kwenye mtandao na mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Kilimo Hussein Bashe.
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakaniÂ
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best