Na David John TimesMajira Online
WANAHARAKATI wa kupinga ukatili wa kijinsia nchini Tanzania wametambuliwa na Umoja wa Ulaya kwa kupewa tuzo kama ishara ya kuthamani kazi wanayoifanya huku ikielezwa kuwa mapambano dhidi ya vita wa ukatikli wa kijinsia ni ya kila mmoja wetu.
Tuzo hizo zimetolewa Dar es Salaam na kushuhudia wadau kutoka mashirika,sekta binafsi,wadau wa kupinga ukatili pamoja na mabalozi mbalimbali wanaowakilisha nchi zao hapa nchini ambazo zipo kwenye umoja huo.
Akizungumza wakati wa tukio hilo la utoaji tuzo, Balozi wa Umoja wa Ulaya Fant amesema kuwa Dunia ipo katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia na hivyo mataifa yote yanapaswa kuungana katika mapambano haya.
“Mapambano haya sio Tanzania pekee ila ni ulimwengu mzima, wote hivyo ni lazima tuungane kwa pamoja kuhakikisha ukatili wa kijinsia unapungua kwa kiasi kikubwa” Amesema Balozi Fanti.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Utamaduni Ubalozi wa Ufansa Cecile Frobert amezungumzia Tamasha la hisani la kupinga ukatili wa Kijinsia lililoambatana na utoaji wa Tuzo mbalimbali kwa watu binafsi na Taasisi zilizoshiriki katika kutoa mchango wao kukomesha vitendo vya ukatili wa Kijinsia hapa nchini ambapo wasanii walioshiriki Tamasha hilo waliimba nyimbo za jamii kupinga ukatili wa kijinsia.
Vinara hao licha ya kupatiwa Tuzo hizo pia walipata fursa ya kuzungumzia kazi zao wanazozifanya zilizowapelekea kufikia hatua hiyo.
Joyce Kiyango ni miongoni mwa watu waliopata Tuzo hizo ambapo akizungumzia tuzo hiyo amesema kuwa hilo limetokana na ubunifu alioufanya kufundishia wanafunzi wake nakwamba ubunifu huo umemuwezesha kuzaa matunda kutokana na watoto wake kupenda masomo darasni na kuondoa kabisa tatizo la utoro.
“Nimejisikia furaha sana kupata Tuzo hii mana hiki ni kitu ambacho nilikua nafanya tu ili watoto wapende masomo lakini sikutegemea kama ingenifanya kufahamika na kufikia hapa leo, kwakweli imenipa faraja sana” amesema Joyce.
More Stories
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa