Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online, Dar es Salaam
KITUO Cha Sheria za Haki za Binadamu (LHRC) kimeiomba Serikali pamoja na wadau wa habari kutoa maoni ya kina yatakayochangia kuboreshwa kwa sheria za habari na upatikanaji wa taarifa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mwishoni mwa wiki Mkurungezi wa LHRC , Anna Henga wakati akitoa pongezi kwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nauye kwa kufungua mlango wa majadiliano ya kuboresha sheria ya Habari.
“Tamko la Waziri Nape la kuyafungulia magazeti yalikuwa yamefugiwa imekua ni kiashiria kizuri cha kurudi kwa uhuru wa vyombo vya habari, hivyo ni muda muafaka sasa wa kuangalia changamoto za kiujumla za sheria inayoikabiki Sekta ya habari na uhuru wa kujieleza”amesema Henga
Amesema kuwa, sheria za habari zilizopo kwa sasa bado zinaendelea kuumiza haki ya kupata taarifa kama ilivyoainishwa katika ibara ya 18 ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ambapo athari yake imeathiri magazeti, Radio, Television,mitandao ya kijamii na uhuru wa internet.
Mkurungezi huyo amesema LHRC imekua ni mdau mkubwa wa habari sheria za habari ambapo imekua ikifanya uchechemuzi kwa muda mrefu tangu kuibuka kwa wimbi la utungaji wa sheria zinazoweka ugumu kwa vyombo vya habari kufanya kazi zake, piah kwa kiwango kikubwa sheria hizo zimekwamisha urahisi wa upatikanaji wa taarifa kwa jamii.
“Tumeshuhudia kurejeshwa kwa leseni za magazeti manne ikiwemo gazeti la Mwanahalisi lenye namba 0000433, Mawio lenye leseni namba 0000437, Mseto lenye leseni namba 0000436 na Tanzania Daima lenye leseni namba 0000434, kufuatia maelekezo ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan”amesema Henga.
Alibainisha miongoni mwa sheria zinazokwamishwa kuwepo kwa uhuru wa habari ni pamoja na sheria ya makosa ya mtandao, ya mwaka 2015 , Sheria ya upatikanaji wa habari ya mwaka 2016, sheria ya mamlaka ya mawasiliano pamoja na kanuni zake, na sheria ya huduma ya vyombo vya habari ya mwaka 2016.
Hata hivyo, amesema wanaimani na Serikali kwamba itaendelea na jitihada za kukuza na kuendeleza na uhuru wa vyombo vya habari kwa maslahi na ulinzi wa waandishi wa habari pamoja na kudhibiti ufungiaji holela wa vyombo vya habari, pamoja na kuweka mazingira rafiki Ili kurejesha hali ya uchumi wa vyombo vya habari vilivyoathirika na sheria hizo.
More Stories
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili
ACT-Wazalendo,waitaka Polisi kutobeba chama kimoja