WANAFUNZI wa kike wa shule za Sekondari Mighareni na Kwakoko wilayani Same Mjini,mkoani Kilimanjaro,wamepatiwa taulo za kike bure zenye thamani ya Sh700,000/= (laki saba) ziwawezeshe kupunguza adha ya kushindwa kuhudhuria darasani wakati wa hedhi.
Baadhi ya wanafunzi wanaotoka katika shule hizo,wamekuwa wakishindwa kuhudhuria baadhi ya vipindi darasani wawapo katika kipindi cha hedhi kwa kukosa taulo za kike na kupelekea utolo na kudhoofisha taaluma yao na kushindwa kufikia ndoto zao kielimu.
Akikabidhi taulo za kike kwa baadhi ya wanafunzi wa shule za Mighareni na kwakoko,Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro,Kasilda Mgeni ambaye alikuwa mgeni rasmi amewataka wananfuzi hao kujiepusha na masuala yanayopelekea mmomonyoko wa maadali wawapo nyumbani na kujikuta baadhi yao kushindwa kufikia ndoto kwenye masomo.
“Sisi Wanawake tunauwezo mkubwa sana lakini jitahidini sana kujiepusha na mambo yatakayowafanya msifikie ndoto zenu kwahiyo niwaombe sana mnapokuwa Shuleni someni…fanyeni kile kilicho waleta Shuleni wazazi wenu wanawategemea sana…. Chonde chonde wanangu someni hayo mambo mengine mtakutana nayo baadae,”amesema Mgeni.
Aidha Mkuu huyo wa wilaya amewasisitiza wanafunzi hao kuitumia vyema fursa iliyotolewa na Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya Elimu bure kuanzia ngazi ya Msingi hadi Sekondari.
Nao baadhi ya baadhi ya wanafunzi mabinti wanaosoma shule hizo wamesema baadhi yao wanashindwa kuhudhuria vipindi darasani kwa kukosa taulo za kike ambapo huwalazimu kubaki nyumbani mapaka siku zao za hedhi zitakapokwisha.
Jenipher Mgonja,mmoja wa wanafunzi wa shule ya Mighareni,alisema changamoto ya kukosa taulo za kike inapelekea wanafunzi kuwa watoro darasani na kushindwa kwenda shule na kuwalazimu kubaki nyumbani kwa kukosa msaada wa kujisitiri.
“Tunamshukuru Mkuu wa wilaya ya Same,watumishi wanawake kutoka Ofisi ya Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya ya Same pamoja na wadau kutoka Mashirika yasiyo ya Kiserikali kwa kutupatia taulo za kike ,kwani kabla ya hapo tulipata changamoto mbalimbal.wengine walishindwa kuhudhuria vipindi darasani kwa kukoso taulo za kike” amesema.
Zoezi hilo la utoaji wa taulo hizo ilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake ambapo watumishi wanawake kutoka Ofisi ya Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya ya Same pamoja na wadau wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali waliguswa na kuchangia taulo za kike kumuwezesha mtoto wa kike kuweza kufikia malengo yake ya kielimu na kuhudhuria masomo kikamilifu.
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu