Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbeya
WATOTO watano waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu waliopelekwa masomoni nchini Nigeria kwa ufadhili wa Taasisi ya Tulia Trust wamewasili nchini jana na kupokelewa katika uwanja wa Ndege wa Songwe tangu mwaka 2018.
Wanafunzi hao walifadhiliwa masomo na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo ,Spika wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini ambaye pia ni Rais umoja wa Mabunge Duniani (IPU)Dkt.Tulia Ackson .
Akizungumza na waandishi wa habari Agosti 16 mwaka huu mara baada ya mapokezi mmoja wa wanufaika wa ufadhiri huo ,Beauty Mwasolokoto amesema wanamfananisha Dkt ,Tulia kama Mshumaa unaowaka na kumulika mwanga mpaka unaisha.
“Mtu hawezi kuwa kiongozi kama hawezi kuwa na maamuzi ya kuacha vitu vyake vyote na kuweka watu wengine mbele hivyo Ndugu zetu watanzania tunaomba msaidieni Dkt.Tulia ni mtu anayeshika wasiojiweza na kuwanyanyua ili waweze kusonga mbele”amesema mmoja wa watoto hao Beauty Mwasolokoto.
Mwanafunzi mwingine Ayubu Mwaihola amesema kuwa Dkt.Tulia amekuwa msaada kwa wananchi wasiojiweza wakiwemo wanafunzi ambao uhitaji wao bado ni changamoto.
“Dkt.Tulia ametuongezea sisi ambao tulikuwa tuna maisha magumu kule kuvaa,kula,kulala vyote vilikuwa vigumu nikikumbuka niliambiwa Baba yangu alikufa kabla sijazaliwa kwa hiyo simjui baba nimelelewa na Mama ,kaka na Dada kwenda shule ilikuwa vigumu kutokana na mazingira magumu ya nyumbani,lakini Dkt Tulia alijitoa kunipeleka nchini Nigeria kusoma kuanzia kidato cha kwanza mpaka sita mpaka nimemaliza na kufaulu vizuri”amesema Ayub.
Kwa upande wake Meneja wa Taasisi ya Tulia Trust,Jackline Boaz amesema kuwa Dkt.Tulia aliwapeleka masomoni nchini Nigeria watoto watano ambao wanatoka katika mazingira kutoka mkoa wa Mbeya na Ruvuma.
“Leo tumekuja kuwapokea watoto wetu watano baada ya kumaliza masomo yao kwa muda wa miaka sita waliyo kaa huko nchini Nigeria ambapo walienda 2018 ,wakiwa wanaenda kuanza kidato cha kwanza na Sasa ni 2024 wamemaliza kidato cha sita hivi Sasa wamerudi kwa mapumZiko mafupi wararudi tena kwa ajili ya kwenda chuoni”amesema Meneja huyo .
Watoto waliopelekwa masomoni kwa ufadhili wa Tulia Trust chini ya mkurugenzi wake Dkt.Tulia Ackson ni Anna Shitindi ,Bernada Fuine ,Beautiful Mwasolokoto,Ayubu Mwaihola,
Suzana Mwakilima .
Baada ya mapokezi hayo walifika shule ya Sekondari ya Tulia Girl’s na Dkt.Tulia Sekondari na kukabidhi msaada wa MADAFTARI kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika Shule hizo ikiwa ni sehemu ya shukrani kwao kwa watoto wenzao wanaoishi katika mazingira magumu.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa