Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
Wanafunzi waliosoma Tanga School Alumni Association, wanatarajia kufanya mkutano mkuu October 28 mwaka huu utakaofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere.
Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa (TSAA) Meja Generali Mstaafu Hamisi Semfuko, alisema mkutano huo ni sehemu ya utekelezaji wa Katiba ya umoja huo ambapo pamoja na mambo mengine watafanya uchaguzi wa viongozi wa kudumu wa umoja wao .
“Wanafunzi wote tuliosoma Tanga School Alumni Associotion tunatarajia kufanya mkutano mkuu wa kikatiba wa umoja wetu wenye lengo la kuchagua viongozi wa kudumu wa umoja ambapo wanafunzi mbalimbali waliosoma shule hiyo wataluwepo akiwemo Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na wengine waliosoma Tanga school watakuwepo wageni mbali mbali akiwemo Mkuu wa mkoa Tanga na viongozi wa jiji la Tanga ,wabunge na wadau muhimu wa umoja huo.
Meja Generali Mstaafu Hamisi Semfuko, Mwenyekiti wa umoja huo alisema mgeni rasmi siku hiyo Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Ummy Mwalimu Mbunge wa Tanga .
Alisema umoja huo ulikuwa ukiitwa kwa jina la shule ya sekondari Tanga maarufu Tanga School umesajiliwa mwaka 2022 ambapo madhumuni ya umoja huo kuwaunganisha watu wote waliosoma Tanga school kuanzia mwaka 1960 mpaka mwaka jana pamoja na wadau muhimu wa shule hiyo kwa ajili ya kuieneza historia ya Elimu.
Katibu wa umoja huo, Godwin Mbaga, alisema dhumuni lingine la umoja huo na lengo kuu kuieneza historia ya elimu
Katibu Godwini Mbaga alisema umoja huo pia unalenga kuunganisha nguvu na kuweka jitihada za pamoja katika kuboresha kiwango cha taaluma kwenye shule hiyo na kuwahamasisha watanzania juu ya umuhimu wa kuenzi elimu ya sekondari nchini iliyoasisiwa mkoni Tanga enzi za Utawala wa ujerumani .
Aidha alisema majengo ya Tanga school kwa sasa yanajulikana kwa jina ( Old Tanga school )yaliojengwa na chama cha Kikoloni cha Wajerumani mwaka 1895 eneo la Mkwakwani mjini Tanga ikiwa ni Kituo cha elimu kwa Vijana wa kiume na mafunzo ya Ualimu ,baadae mwaka 1905 iliidhinishwa rasmi shule ya sekondari na walimu wengi walikuwa walimu ni wageni na iliendelea kutoa elimu ya sekondari kwa vijana wa kiume wa Tanganyika mpaka baada ya uhuru.
Mbaga alisema mwaka 1972 ilibadilishwa na kuwa shule ya sekondari ya Ufundi kwa Wavulana pekee na mnamo mwaka 1988 Serikali ya Tanzania ilianzisha masomo ya sekondari , sekondari kwa wasichana na kuifanya shule kuwa jinsia Mchanganyiko baada ujenzi wa mabweni mapya ya wasichana mpaka hivi sasa Tanga School imekuwa ni shule ya wanafunzi wa jinsia Mchanganyiko
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu