Na Mwandishi wetu ,Timesmajira
WANAFUNZI wa shule huria ya Ukonga Skillfull wametakiwa kuishi katika ndoto zao na kuonesha vipaji vyao ambavyo Mungu amewapa katika kuwaletea mafanikio makubwa katika maisha yao.
Akizungumza juzi jijini Dar es Salaam,wakati wa mahafali ya 19 ya Shule hiyo ya Kidato cha Sita,Mwalimu wa Shule Binafsi,Irene Muthemba ambaye ni mgeni rasmi wa Mahafali hiyo,alisema kusoma kwa bidii na kujituma katika ndoto za wanafunzi hao ndio msingi wa kuwafisha katika mafanikio na kufika mbali zaidi.
Amesema wanafunzi wa shule hiyo wanatakiwa kukaa na kuishi ndani ya Mungu kwani yeye ndiye mlinzi wa kila kitu.”Someni kwa bidii akisema elimu ni agizo kutoka kwa Mungu kwamba watakuwa na msingi mzuri katika maisha.
“Nawapa hongera wahitimu kwa kuamua kusoma na kufika hapo malipo, Mungu azidi kubariki kazi ya mikono yenu,”Msikate tamaa, ishi ndoto zenu onesheni vipaji ambavyo Mungu amewapa viwaletee mafanikio na hatimaye mtafanikiwa. Hata Nassibu Abdul ‘Diamond platnumz’ mafanikio hayakuja kwa haraka kama mnavyomuona alipambana,”amesema.
Kwa upande wake Muasisi na Mkurugenzi wa Shule hiyo huria ya Ukonga Skillfull,Diodorus Tabaro amesema wanafunzi wanaohitimu kidato cha sita kwa Shule hiyo ni takribani 79 ambao wanatarajia kufanya mtihani wao wa kumaliza shule kuanzia Mei 5,2025 katika michepuo ya Sayansi,Sanaa na Biashara.

Amesema shule yao ya huria inamakundi mawili wanaohitimu shule kwa kidato cha sita ikiwemo wanafunzi walikuja shule mwaka 2022 ambao tayari walikuwa wanataka kurudia mtihani wao wa taifa wa kidato cha nne walifanikiwa na kupata matokeo ya kupata kidato cha tano na kundi lingine kutoka shule nyingine binafsi na kujiunga moja kwa moja kidato cha tano.
“Mwakani tunatimiza miaka 20 ya kuanzishwa kwa shule hii huria ambayo itaenda tutakuwa na kumbukizi ya uwepo wa Ukongo Skillull tangu kuanzishwa kwake mwaka 2016 kuelekea 2026.
“Tutawakusanya wanafunzi wetu wote ambao wanadegree zaidi ya 700 pamoja na wale wenye diploma na vyeti,”amesisitiza Tabaro.
Mbali na hiyo amesema ifike muda shule huria zifike wakati wa kuona wanaweza kuwasaidia vijana na sio kuonekana kama shule za kihuni. “Shule huria ni kama shule yoyote ya kawaida ni namna ya ufundishaji na watu gani wanaohudumia,uwepo wa Ukonga Skillfull imeleta Chachu kubwa sana ya mabadiliko katika utoaji wa elimu katika shule huria tumefanya vizuri sana na tunaaminika na kuwa mfano kwa wengine.
“Pia wazazi wawe kawaida kukagua shule hizo ila kwa sasa hivi shule zinaaminika na tunapokea wanafunzi wengi kutoka shule za kawaida na kujiunga na shule huria,”amesema Tabaro.
Naye Mkuu wa shule hiyo Allen Tibaigana amesema wahitimu hao wamekuwa na historia tofauti wengi walikuwa wamefeli darasa la saba, wengine walifeli kidato cha nne na kurudia walikwenda wakiwa wamekata tamaa lakini wao waliwatengeneza kwa kuwandaa kisaikolojia na anaamini watafanya vizuri
More Stories
Mshama:Vijana jitokezeni mzunguko wa pili wa uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapigakura
Serikali yaombwa kusambaza umeme kwa kasi na kuboresha huduma vijijini
Rais Samia ateua Wenyeviti bodi mbalimbali