November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wanafunzi shule ya  msingi Salsasha watembelea bunge kujifunza kwa vitendo

Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma

SHULE ya Awali na Msingi Salsasha iliyopo mkoa wa Morogoro imetembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,jijini Dodoma wakiwa na lengo la kujifunza jinsi shughuli za bunge zinavyoendeshwa kwa maslahi ya taifa.

Akizungumza kwenye viwanja vya Bunge mara baada ya kutoka kwenye mkutano wa 15,kikao cha kwanza leo,Aprili 2,2024 Mwalimu Mkuu Kiongozi wa shule hiyo Abduswamadu Wahabu Balala amesema kuwa madhumuni ya ziara hiyo bungeni ni walimu pamoja na wanafunzi 23 walioongozana nao kwenda kujifunza kwa vitendo shughuli za kibunge kwani wanafunzi hao ndiyo viongozi wa baadae.

“Tuanatarajia hawa watoto ndiyo watakuwa viongozi wa baadae ambao watakuja kutupambania na kupigania taifa kwa ujumla na leo wameona wenyewe
namna gani spika anavyoendesha shughuli za Bunge,namna gani wabunge wanavyochangia michango yao.

“Lakini kwanini wanachangia michango yao ili kuweza kulisaidia taifa letu lakini pia wabunge wameweza kueleza changamoto ambazo zinakumba majimbo yao na hizo changamoto zakupatiwa majibu .

“Kwahivyo sasa kwa hiki kizazi ambacho tupo nacho kama mtoto mdogo ataweza kuja kujifunza kuona namnagani changamoto ambazo zipo kwenye jamii zivyowasilishwa kwahiyo itamsaidia na kumjenga katika uwezo wake hapo baadae kuja kuwa balozi mzuri wa kusaidia taifa hili,”amesema Mwalimu Mkuu.

Kwaupande wake mwanafunzi Ashrafu Miraji anayesoma darasa la tatu katika shule hiyo ameeleza furaha yake baada ya kuja bungeni ambapo amesema amefurahi kumuona Spika ,Dkt Tulia Ackson na viongozi wengine mbalimbali .

Naye mwanafunzi Salwa Twaha amesema kuwa amejisikia furaha kufika bungeni kwani alikuwa anamuona Spika kwenye television lakini leo amemuona anakwa ana na amejifunza ujasiri wake wa kuongoza bunge.

Sabra Kibwana mmiliki wa shule ya awal8 na msingi Salsasha ameeleza kuwa hata yeye ni mara yake ya kwanza kufika bungeni hivyo ameona vitu vingi vya kumjenga kama kiongozi wa shule yake atakuongeza na alivyonavyo.

“Vile ambavyo ninavyo nitazidi kuongeza kwasababu huku nimeona vitu vingi zaidi watu wanaujasiri,watu wanaweza kufanya yani mtu anafanyakitu anajiamini anaongea kwa kujiamini anahisi hiki ninachokifanya niongeze ufundi .

“Na mimi nilivyokuja huku nimekuja na watoto lakini kuja kwao hapa wamejifunza kitu japo ni wadogo wa darasa la tatu na la nne lakini kwa walichokiona hapa ninauhakika kwenye safari ya kurudi watauliza vitu vingi wakitaka majibu kwa ujasiri walioupata kwa wabunge wakiuliza maswali lakini jinsi tulivyowajenga wanajua kujieleza hivyo walivyojifunza hapa hata nyumbani wataeleza kama vilivyo,”amesema Kibwana.