Na Heri Shaaban,Timesmajiraonline,Ilala
WANAFUNZI wa shule ya Msingi Ilala Boma wilayani Ilala wamefanya ziara ya masomo katika uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere .
Akizungumza katika ziara hiyo mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Ilala Boma Endrew Koti alisema dhumuni la ziara hiyo kuwajengea uwezo Wanafunzi wa shule hiyo waweze kujiamini kwa kuwa wanajifunza kwa vitendo.
“Shule yetu ya msingi Ilala Boma imekuwa ikifanya ziara kwa vitendo katika taasisi za Serikali kuwapeleka Wanafunzi sehemu mbalimbali kwa lengo la kukuza taaluma Wanafunzi ziara za awali tuliwapeleka Chuo Kikuu cha Afya Muhimbili (MUHAS )kwa ajili ya kujifunza ,Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) na ziara ya leo hii Uwanja Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere lengo kuwanda Wanafunzi kwa ajili ya ndoto zao za kesho wanafunzi wanaotaka masuala ya afya walifika chuo cha afya Muhimbili (MUHAS) wakajifunza na wale wanaotaka maswala ya Rubani kurusha ndege wamefika uwanja ndege na wamejifunza”alisema Endrew.
Mwalimu Endrew Koti, alisema Mtaala mpya Competence Based Curriculum (CBC)unalenga zaidi kukuza ujuzi ,maarifa,na mwelekeo kwa mwanafunzi badala kuzingatia alama za mitihani .
Aidha alisema mwanafunzi anahitaji kuwa mshiriki wa kazi na siyo mpokeaji tuu wa maarifa anapaswa kushiriki kikamilifu kwenye mazoezi ,mijadala na miradi ya vitendo ili afanikiwe awe na hoja za uhakika na kijiamini apate fursa ya kutembelea mazingira yatakayojenga na kuimalisha udadisi.
“Ziara hizi tunazofanya na wanafunzi wetu kujifunza kwa vitendo mfano kupitia maabara ,kazi za mikono michezo ya kuigiza yote hayo ukimpa mwanafunzi swali la kuandika INSHA anaweza kujaza ukurasa zaidi ya hata tano kwa wingi wa taarifa alizokusanya .
Akizungumzia kitaaluma alisema shule ya msingi Ilala Boma kila mwaka inafanya vizuri wanafunzi katika kipindi cha miaka mitatu wanafunzi wanafaulu kwa asilimia 100 kwenda kidato cha kwanza na mwaka huu mikakati ya shule hiyo wanafunzi wote wanatarajia kufanya mitihani yao ya Taifa watafaulu kwa asilimia 100 kutokana na kuandaliwa vizuri na walimu wa shule hiyo kwa kushirikiana na Wazazi wao.




More Stories
Nishati ya umeme jua kupunguza gharama za uzalishaji migodini
Rais Samia atoa bil.10 ukarabati barabara za ndani Ilala
Diwani aeleza mafanikio yake Kata ya Bonyokwa