December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wanafunzi 95224 wamaliza darasa saba Dar es Salaam

Na Herishaban, TimesMajira Online, Ilala

Jumla ya wanafunzi 95224 wamefanya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi mkoa Dar es Salaam kwa utulivu.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam Afisa Elimu mkoa Dar es Salaam Mwalimu Alhaj Abubakari Mauld alisema kati ya wanafunzi 95224 wavulana idadi yao 46543 na wasichana 48681.

“Jumla ya shule 776 za mkoa Dar es Salaam wanafunzi wamefanya mitihani yao ya kumaliza elimu ya msingi kwa utulivu Mkoa tumejipanga vizuri kwa siku zote mbili kwa kushirikiana na Ofisi ya mkuu wa mkoa Dar es Salaam “alisema Alhaj Maulid.

Mwalimu Maulid alisema katika mkoa huo jumla ya wanafunzi 171 pia wamefanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka huu 2023 katika shule tofauti za Serikali zilizopo Dar es Salaam.

Aidha alisema kati ya wanafunzi hao 95224 wa mkoa wilaya ya Ilala wamefanya mtihani wanafunzi 33547 wilaya ya Kinondoni ,na wanafunzi 14925 Wilaya ya Ubungo 16683 ,Wilaya ya Temeke 24662, na Wilaya ya Kigamboni 5407.