Na Herishaban, TimesMajira Online, Ilala
Serikali ya Mtaa Kalume imetoa chakula bure cha wanafunzi wa 208 wa darasa la saba wanaomaliza elimu ya msingi shule ya msingi Ilala Boma na Mkoani .
Akizungumza wakati wa kugawa chakula kwa wanafunzi wa shule ya Ilala Boma Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Kalume Hajji Bechina, alisema utaratibu wa kulisha chakula bure kwa wanafunzi kwa shule ya Ilala Boma na Mkoani ni endelevu kila mwaka .
“Serikali ya mtaa Kalume Ilala kwa kushirikiana na chama cha Mapunduzi CCM tawi la Shauri moyo tumeweka utaratibu wetu wa kulisha chakula bure shule za kata ya Ilala ,Ilala Boma na Mkoani kugawa chakula bure kila mwaka katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan “alisema Bechina
Mwenyekiti Bechina alisema Serikal ya Mtaa Kalume imewapunguzia Wazazi mzigo watoto wao siku mbili za mitihani wanakula chakula bure kinachogharamia na Ofisi ya Serikali ya Mtaa kuanzia chai asubuhi na chakula cha mchana kila mwaka.
MWENYEKITI BECHINA aliwatakia khery wahitimu wa darasa la saba wanaomaliza elimu ya msingi katika shule hizo mbili za kata ya Ilala katika mitihani yao ya kuhitimu ekimu ya msingi.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua