Na Bahati Sonda,TimesMajira Online,Simiyu
WANAFUNZI 1,837 sawa na asilimia 6.7 ya waliofaulu ambao ni 27,433 wamekosa nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza 2021 katika mkoa huo kutokana na ukosefu wa vyumba vya madarasa 155.
Katibu Tawala Mkoa huo, Miriam Mmbaga amesema kuwa wanafunzi waliopata nafasi, wavulana ni 12,116 huku wasichana wakiwa 13,480.
Aidha ambao hawakupata nafasi katika awamu hii ya kwanza ya uchaguzi, wavulana ni 635 na wasichana ni 1,202 ambao wanatoka Wilaya ya Bariadi 948, Itilima 162 na Meatu 707,” amesema Katibu tawala.
Hata hivyo amewataka wakurugenzi na viongozi wengine wa halmashuari ambazo zinatakiwa kujenga vyumba hivyo vya madarasa, kuhakikisha wanaendelea na ujenzi huo ili ukamilike kwa haraka, ili ifikapo Februari mosi, 2021 wanafunzi hao waweze kuanza.
Awali akitoa taarifa ya ukosefu wa vyumba hivyo vya madarasa, Afisa elimu Mkoa, Erenest Hinju amesema kuwa Wilaya ya Bariadi vijijini wanahitaji vyumba 54, Bariadi mji 30, Itilima 22, Maswa 10, Meatu 39 huku Wilaya ya Busega ikiwa haina changamoto hiyo.
Jumla ya wanafunzi 25,596 sawa na asilimia 93 ya wanafunzi wote waliofaulu mtihani wa darasa la saba mwaka 2020 katika mkoa wa Simiyu, wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2021.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua